Ureno Yafuzu Fainali ya UEFA Nations League kwa Kuifunga Ujerumani | Cristiano Ronaldo anaiongoza Ureno kutinga fainali ya UEFA Nations League akiwa amefunga bao lake la 937
Nyota wa soka duniani Cristiano Ronaldo ameweka historia baada ya kufunga bao lake la 937 katika maisha yake ya soka, na kuiwezesha Ureno kufuzu kwa fainali za UEFA Nations League kwa ushindi wa 2-1 dhidi ya Ujerumani.
Katika mchezo wa nusu fainali usiku wa jana, Ujerumani ilitangulia kwa bao la Florian Wirtz dakika ya 48, kabla ya Francisco Conceição kuisawazishia Ureno dakika ya 63. Dakika tano tu baadaye, Ronaldo alifunga bao la ushindi dakika ya 68, na kuifanya Ureno kukaribia kutwaa taji la Uropa.
Kwa matokeo haya, Ureno sasa inasubiri mshindi wa nusu fainali ya pili kati ya Uhispania na Ufaransa, ambayo itamenyana kesho katika vita vingine vikali vya kuwania kufuzu fainali.

Ureno Yafuzu Fainali ya UEFA Nations League kwa Kuifunga Ujerumani
FT: Ujerumani 1-2 Ureno
48’ Wirtz F.
63’ Conceicao F.
68’ Ronaldo C.
CHECK ALSO:
Weka maoni yako