Ureno Yafuzu Kombe la Dunia 2026 Kwa Kishindo, Ureno Yaonyesha Ubabe, Yafuzu Kombe la Dunia 2026 Kwa Ushindi wa 9β1 Dhidi ya Armenia.
Timu ya taifa ya Ureno imeweka rekodi ya kipekee katika hatua ya kuwania kufuzu Kombe la Dunia la FIFA 2026 baada ya kuibamiza Armenia kwa ushindi mnono wa mabao 9β1. Mchezo huu umeshuhudia uwezo mkubwa wa kikosi cha Ureno ambacho kimehakikisha kinapata tiketi ya kushiriki fainali za Kombe la Dunia zitakazofanyika Marekani, Mexico na Canada.
Ureno Yafuzu Kombe la Dunia 2026 Kwa Kishindo
Katika mchezo huo, nyota wawili, Bruno Fernandes na JoΓ£o Neves, waliibuka mashujaa kwa kufunga hat-trick, wakionyesha kiwango cha juu na ubora wa safu ya kiungo ya timu hiyo.
Magoli
Portugal π΅πΉ
-
07β β Veiga
-
28β β Ramos
-
30β β JoΓ£o Neves
-
41β β JoΓ£o Neves
-
45+3β β Bruno Fernandes (Penalti)
-
52β β Bruno Fernandes
-
72β β Bruno Fernandes (Penalti)
-
81β β JoΓ£o Neves
-
90+2β β ConceiΓ§Γ£o

Armenia π¦π²
-
18β β Spertsyan
Ureno Yapata Tiketi Rasmi ya Kombe la Dunia 2026
Kwa ushindi huu mkubwa, Ureno imejihakikishia nafasi kwenye fainali zijazo. Ushindi wa 9β1 unaonyesha kiwango chake bora na matarajio makubwa kuelekea mashindano yajayo.
Kikosi hicho kinaonekana kuwa na uimara katika viungo, kasi katika mashambulizi, na mfumo thabiti wa ulinzi β viashiria muhimu kwa timu inayotaka kufika mbali katika fainali zijazo.
CHECK ALSO:








Weka maoni yako