Usajili Mpya wa Simba SC 2025/2026, Usajili Simba Leo, Wachezaji Wanaotakiwa Msimbazi | Dirisha Kubwa la Usajili Ligi Kuu Bara 2025/2026: Simba Waanza Harakati za Usajili.
Kipindi cha usajili wa dirisha kubwa Ligi Kuu Tanzania Bara kinakaribia kufunguliwa, tayari vigogo wa soka nchini, Simba SC na Yanga SC, wameanza kuweka mikakati ya kuimarisha vikosi vyao kuelekea msimu ujao wa mashindano ya kimataifa.
Kwa mujibu wa chanzo makini, kuna vuguvugu la ndani kati ya klabu hizo mbili kubwa nchini, zikihusisha kusaka wachezaji kutoka Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC), taifa lenye vipaji vingi vya soka.
Kwa sasa Ligi Kuu Bara inathibitisha kuwa Simba na Yanga zitaiwakilisha Tanzania Bara katika michuano ya Ligi ya Mabingwa Afrika msimu wa 2025/2026, huku Singida Black Stars na Azam FC zikitarajiwa kushiriki Kombe la Shirikisho Afrika.
Usajili Mpya wa Simba SC 2025/2026

Waliosajiliwa Mpaka sasa Simba
Wafuatao ni wachezzaji waliokamilisha usajili wa kujiunga na Simba kwa msimu mpya wa mashindano wa 2025/26:-
- Wilson Nangu – kutoka JKT Tanzania
- Morice Abraham – Kutoka FK Spartak Subotica
- Alassane Kanté – Kutoka CA Bizertin
- Rushine De Reuck (29) – Mamelodi Sundowns
- Charles Daud Semfuko 🇹🇿 – Coastal Union
- Neon Maema (29) – Mamelodi Sundowns
- Abdallah ‘Zambo Jr’ – Coastal Union
Kuhakikisha mafanikio katika mashindano ya kimataifa kunahitaji uwekezaji wa mapema katika usajili wa nguvu, unaozingatia ubora wa wachezaji, uzoefu wao, na uwezo wa kushindana kwa kiwango cha juu. Kwa hiyo, Simba na Yanga zinasaka vipaji kutoka DRC, taifa ambalo limekuwa na ushawishi mkubwa barani Afrika kwa kuzalisha wachezaji wa kiwango cha juu.
CHECK ALSO:
Wapinzani wajiandae simba ijayo… nisiwe msemaje watajionea.