Usajili Simba Leo Dirisha Dogo, Dondoo za Usajili Simba Leo, Dirisha Dogo 2025/26 TETESI za Usajili wa Simba SC 2025/26 Dirisha Dogo | Wachezaji waliosajiliwa na Simba kwenye dirisha dogo la usajili 2025/2026.
Mpaka sasa baada ya dirisha dogo la usajili la msimu wa 2025/2026 kufunguliwa, yapo majina yanayotajwa kutua kwenye kikosi cha Simba kuongeza nguvu na kuipambania nembo ya wanasimba.
Usajili Simba Leo Dirisha Dogo
Haya hapa baadhi ya majina yanayoitajika kutua kwenye kikosi cha Simba kwenye dirisha dogo la usajili/Usajili Simba Leo Dirisha Dogo:-

01. Samba O’Neil (25)
Beki wa kati na nahodha wa Asante Kotoko 🇬🇭, Samba O’Neil (25) yupo kwenye rada za Simba SC. Bingwa wa kupiga vichwa Kambani, mkali wa kukaba na mwenye uzoefu mkubwa Kwenye safu ya ulinzi.
Simba inalenga kuongeza nguvu kwenye safu ya ulinzi kuelekea vita ya CAF Champions League 🏆 na Ligi Kuu Tanzania 🇹🇿, huku O’Neil akitajwa kama mbadala sahihi endapo Chamou Karaboue ataondoka.
02. KHADIM DIAW
Inaelezwa klabu ya SIMBA SC imeanza mazungumzo na beki wa zamani wa AL-HILAL OMDURMAN, KHADIM DIAW (27) kwa ajili ya kumsajili katika dirisha dogo la usajili mwezi Januari 2026.
Tetesi zilizopo ni kwamba DIAW amepokea ofa kutoka klabu tatu barani Afrika ambazo ni SIMBA SC, USM ALGER na JS KABYLIE ya ALGERIA…. KHADIM DIAW, ambaye aliwahi kuchezea HOROYA AC na AL-HILAL OMDURMAN, kwa sasa ni mchezaji huru anayeweza kusajiliwa bila vikwazo vyovyote…. Timu itayoweka pesa nzuri kwa DIAW basi uhakika wa kupata huduma yake utakua mkubwa…..✍🏾
03. Dramane Kamagate
Dramane Kamagate (20) nyota raia wa Ivory Coast anayekipiga kwenye klabu ya San Pedro ya huko huko kwao Ivory Coast. Dramane ni mshambuliaji wa kati na moja ya sifa zake ni speed na uhatari mbele ya lango la wapinzani.🔥
Msimu uliopita aliibuka kinara wa ufungaji kwenye ligi ya Ivory Coast (Ligue 1) akifunga jumla ya mabao 11. Na kwenye mechi 5 za mwisho msimu huu amefunga jumla ya goli 5.🔥
04. Idris Diomande
Simba SC ipo kwenye mazungumzo na klabu ya Singida blackstars kwa ajili ya Kumsajili Idriss Diomande.
Idris Diomande kiungo wa kimataifa wa Ivory coast mwenye umri wa miaka 27 alijiunga na Singida blackstars dirisha kubwa la usajili akitokea Zoman FC ya Ivory coast.
05. Chikumbutso Salima
Chikumbutso Salima “ Chikuh “ Mwenye Miaka Ishirini na nne kutokea Nyasa Big Bullets yupo kwenye list ya Rada za viongozi wa Simba wakihitaji saini yake kwenye dirisha hili dogo .
Chikuh ni Top Scorer wa ligi ya Malawi akiwa na magoli 15 ndani ya michezo 28 . Je wanalunyasi watafanikiwa kuinasa hii Saini? Uwanja wa Maoni Uko Wazi.
06. Clatous Chota Chama
Simba SC imeingia kwenye mazungumzo ya kina na kiungo mshambuliaji wa Singida Black Stars, Clatous Chota Chama (34) kwa ajili ya kutaka kumsajili katika dirisha hili la usajili.
Habari zinaeleza kuwa mazungumzo baina ya pande zote mbili yanaendelea vizuri, huku makubaliano ya mwisho yakisubiriwa ni masharti binafsi ya mchezaji huyo kabla ya kusaini na kujiunga rasmi na Simba SC.
WACHEZAJI WALIOPO KWA MAJARIBIO
Charles Ouma
Kiungo wa Kenya Police FC Charles Ouma kwa sasa yupo Dar Es Salaam anafanya mazoezi na Simba SC.
Simba Sports Club inamtazama Charles Ouma Kiungo wa Police Kenya FC kama inaweza kumsajili kwenye dirisha dogo la usajili la mwezi Januari.
Bright Anukani
Kiungo mshambuliaji wa timu ya KCCA FC ya Uganda, Bright Anukani yupo nchini Tanzania akifanya majaribio na Simba SC.
Bright Anukani atacheza mashindano ya MAPINDUZI CUP ambayo yanaendelea visiwani Zanzibar.
CHECK ALSO:








Weka maoni yako