Usajili Singida Black Stars, Wachezaji Walisajiliwa

Usajili Singida Black Stars, Wachezaji Walisajiliwa | Kelvin Kijili Arejea Singida Black Stars Akitokea Simba SC kwa Mkataba wa Miaka Miwili.

Usajili Singida Black Stars, Wachezaji Walisajiliwa

Klabu ya Singida Black Stars imetangaza rasmi kumsajili beki wa kulia Kelvin Kijili kutoka Simba Sports Club kwa mkataba wa miaka miwili.

Mtanzania huyo mwenye umri wa miaka 24 anarejea Singida Black Stars mwaka mmoja tu baada ya kuondoka Simba SC Julai 12, 2024 kwa mkataba wa miaka miwili. Hata hivyo, mkataba huo ulikatishwa mapema, na sasa Kijili anajiunga na timu ya Singida kwa ajili ya msimu mpya wa Ligi Kuu Tanzania Bara.

Usajili Singida Black Stars, Wachezaji Walisajiliwa

Kurejea kwa Kijili kunaleta uzoefu na utulivu kwenye safu ya ulinzi ya Singida Black Stars, hasa ikizingatiwa alishawahi kuichezea timu hiyo na anafahamu vyema mfumo wa klabu hiyo.

Uongozi wa klabu ya Singida Black Stars umeonyesha imani kubwa na uwezo wa Kijili hasa kutokana na uzoefu alioupata akiwa na moja ya klabu kubwa nchini Simba SC.

CHECK ALSO:

  1. Mohammed Kudus Asaini Tottenham kwa Dau la Dola Milioni 55
  2. Taifa Stars Yaingia Kambini, Yaelekea Misri kwa Kambi ya CHAN 2024
  3. Jezi Mpya za Yanga Msimu wa 2025/26 na Ubunifu Mpya
  4. TETESI za Usajili, Khalid Aucho Kusalia Yanga