Usajili wa Fei Toto, Apewa Ofa Kubwa ya Kuongeza Mkataba na Azam

Usajili wa Fei Toto, Apewa Ofa Kubwa ya Kuongeza Mkataba na Azam hadi 2028. Anaonyesha nia yake ya kuondoka

KIUNGO mahiri wa Azam FC, Feisal Salum, ameongezewa mkataba wa miaka miwili, lakini bado hajasaini na kusisitiza kutaka kuondoka klabuni hapo.

Kwa mujibu wa taarifa rasmi, mkataba wa sasa wa Feisal Salum unamalizika Juni 8, 2026. Hata hivyo, Azam FC imeandaa nyongeza ya miezi 24, ambayo itaanza mara baada ya kumalizika, kuanzia Juni 9, 2026 hadi Juni 8, 2028.

Usajili wa Fei Toto, Apewa Ofa Kubwa ya Kuongeza Mkataba na Azam

Katika ofa hiyo mpya, Azam FC imemwandalia Feisal Salum masharti yafuatayo:

Usajili wa Fei Toto, Apewa Ofa Kubwa ya Kuongeza Mkataba na Azam
Usajili wa Fei Toto, Apewa Ofa Kubwa ya Kuongeza Mkataba na Azam
  • Ada ya Usajili: Shilingi 805,254,286 za Kitanzania.

  • Malipo Halisi (baada ya kodi): Feisal atapokea kiasi cha TZS 563,850,000.

  • Malipo kwa Awamu: Klabu italipa ada ya usajili kwa awamu mbili.

  • Mshahara: Feisal Salum anatarajiwa kulipwa TZS 79,092,064 kama mshahara wa kawaida.

  • Malipo ya Ziada: Atapokea TZS 50,000,000 baada ya makato ya kodi na NSSF.

  • Makazi: Klabu itampatia nyumba kwa matumizi yake binafsi.

  • Usafiri: Azam FC itatoa tiketi nne za boti kwa msimu mmoja, kwa safari za Dar es Salaam kwenda Zanzibar na kurudi.

  • Kipengele cha Kuachiliwa: Mkataba huo una kipengele kinachoruhusu kuondoka kwa ada ya Dola za Kimarekani milioni 3.

Licha ya ofa hiyo ya kuvutia, Feisal Salum bado hajasaini nyongeza ya mkataba. Ameweka wazi kuwa ana nia ya kuondoka Azam FC huku akiashiria kuwa anaweza kutafuta changamoto nyingine nje ya klabu hiyo kabla ya mkataba wake wa sasa kuisha.

CHECK ALSO: