Usajili Yanga Wachezaji Wanaoondoka, Wanaowaniwa na Wanaoongeza Mikataba | Wachezaji Wanaoondoka Yanga, Waliosajiliwa na Walioongezewa Mikataba Dirisha la Usajili 2025
Yanga SC imeanza kurekebisha orodha yake kabla ya msimu wa 2025/2026. Mabadiliko haya ni pamoja na kuondoka kwa wachezaji kadhaa, mazungumzo na wachezaji wapya, na kuongeza mikataba kwa wachezaji muhimu. Taarifa hizi zinaonyesha hatua za kwanza ambazo uongozi wa klabu unachukua ili kujenga kikosi imara zaidi kwa ajili ya mashindano yajayo.
Usajili Yanga Wachezaji Wanaoondoka, Wanaowaniwa na Wanaoongeza Mikataba
Wachezaji Wanaoondoka Yanga SC
Kufikia sasa, majina yafuatayo yameripotiwa kuondoka ndani ya kikosi cha Yanga SC:
Kennedy Musonda
Desin Nkane
Chama JR
Clement Mzize – Inaripotiwa kuwa anajiunga na timu nyingine zikiwemo Zamalek ya Misri na klabu moja kutoka Ujerumani.
Khomeini Abubakar
Duke Abuya
Khalid Aucho – Hatima yake bado haijafahamika wazi, lakini inategemea iwapo Yanga SC watakubali kumlipa kiasi cha fedha anachodai.
Jonas Mkude
Jonathan IKANGALOMBO

Wachezaji Wanaowaniwa na Yanga SC
Kwa upande wa usajili mpya, Yanga SC imeanza harakati za kusaka nyota wapya watakaoongeza nguvu kikosini. Wachezaji wanaohusishwa na dili za kujiunga na klabu hiyo ni pamoja na:
Arthur Bada
Jonathan Sowah
Célestin Ecua – Dili lake linaelezwa kuwa limefikia asilimia 90 ya kukamilika.
Rhulani Mokwena – Anatajwa kuwania nafasi ya kuwa Kocha Mkuu wa klabu hiyo.
Mohamed Doumbia – Inasemekana tayari amekamilisha makubaliano na Yanga SC.
Wachezaji Wanaoongezewa Mkataba
Aidha, baadhi ya nyota wa kikosi cha sasa wamekuwa wakionyeshwa imani kwa kuongezewa mikataba mipya. Hawa ni:
Dickson Job
Mudathir Yahaya
Pacôme Zouzoua
Maxi Mpia Nzengeli
CHECK ALSO:
Weka maoni yako