Viingilio Ngao ya Jamii 2025, Yanga vs Simba 16/9/2025: SHIRIKISHO la Soka Tanzania (TFF) limetangaza rasmi viingilio vya mchezo wa Ngao ya Jamii, utakaowakutanisha mabingwa watetezi wa Ligi Kuu Bara, Young Africans SC (Yanga) dhidi ya wapinzani wao wa jadi, Simba SC. Mechi hiyo ya kifahari itachezwa Jumanne Septemba 16, 2025, kuanzia saa 11:00 Jioni kwenye Uwanja wa Benjamin Mkapa jijini Dar es Salaam.
Kwa mara nyingine tena mashabiki wa soka nchini watashuhudia pambano la kihistoria litakaloibua msisimko mkubwa na kuzikutanisha klabu kubwa nchini humo. Ngao ya Jamii inatumika kama utangulizi wa msimu mpya kwa kuwakutanisha mabingwa hao wa Ligi Kuu dhidi ya mabingwa wa Kombe la Shirikisho la Azam (FA).
Mashabiki wanahimizwa kununua tikiti zao mapema ili kuzuia mikusanyiko ya watu siku ya mechi, haswa ikizingatiwa kuwa michezo ya watani wa jadi huwavutia watu wengi.
Viingilio Ngao ya Jamii 2025, Yanga vs Simba 16/9/2025
Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na TFF Septemba 14, 2025, bei za tiketi zitakuwa kama ifuatavyo.
- Mzunguko: shilingi 5,000 NT
- VIP C: shilingi 20,000 NT
- VIP B: shilingi 30,000 NT
- VIP A: shilingi 100,000 NT
- Platinum: 100,000 NT shilingi 300,000/=
VIKOSI VYA TIMU
Kikosi cha Yanga
Kikosi cha Simba

Pambano hili linatarajiwa kutoa taswira ya kwanza ya nguvu ya Yanga na Simba kuelekea msimu wa 2025/2026, huku timu zote zikiwa na matumaini ya kuanza kwa ushindi.
CHECK ALSO:
Weka maoni yako