Viingilio vya Mchezo wa Kariakoo Derby Yanga vs Simba | Mashabiki wa soka Tanzania wanatarajia kushuhudia moja ya mechi kali za Ligi Kuu ya NBC inayojulikana kwa jina la Kariakoo Derby kati ya Yanga SC na Simba SC. Mechi hii itachezwa Jumamosi Machi 8, 2025 kwenye Uwanja wa Benjamin Mkapa na itaanza rasmi saa 1:15 usiku.
Viingilio vya Mchezo wa Kariakoo Derby Yanga vs Simba
Tikiti za Mechi
Kwa mashabiki wanaotaka kuhudhuria mchezo huu mzuri, tiketi zimepangwa kama ifuatavyo:
- Mzunguko – TSH 5,000
- Orange – TSH 10,000
- VIP C – TSH 20,000
- VIP B – TSH 30,000
- VIP A – TSH 50,000

Mchezo wa Kariakoo derby umekuwa ni mchezo wa kusisimua unaovutia mashabiki wengi kutokana na uhasama wa kihistoria kati ya wababe hao wa soka. Mechi hii ni muhimu kwa msimamo wa ligi kwani timu zote zinahitaji ushindi ili kujiweka katika mazingira mazuri ya kutwaa ubingwa wa Ligi Kuu ya NBC 2024/2025.
Mashabiki wa soka wajiandae mapema kwa mchezo huu mkubwa kwa kununua tiketi zao mapema ili kuepusha usumbufu wowote. Mechi hii inatarajiwa kuwa na mvuto mkubwa kutokana na historia ndefu ya upinzani kati ya Yanga SC na Simba SC. Uwanja wa Benjamin Mkapa utakuwa katika hali ya mvuto huku mashabiki wakishuhudia pambano la soka kati ya timu bora za Tanzania.
CHECK ALSO:
Weka maoni yako