Vinara wa Clean Sheets Ligi Kuu NBC 2024/25 : Moussa Camara vs Djigui Diarra | Katika msimu wa 2024/25 wa Ligi Kuu Tanzania Bara (NBC Premier League), makipa wawili wanaoongoza kwa clean sheets ni Moussa Camara wa Simba SC na Djigui Diarra wa Yanga SC.
Vinara wa Clean Sheets Ligi Kuu NBC 2024/25
Wote wameonyesha kiwango cha juu kwa kuokoa timu zao katika michezo mingi msimu huu.
Takwimu za Clean Sheets hadi Sasa
🔴 Moussa Camara (Simba SC)
🏟️ Mechi: 20
🧤 Clean Sheets: 15
⚽ Mabao aliyoruhusu: 5

🟡 Djigui Diarra (Yanga SC)
🏟️ Mechi: 16
🧤 Clean Sheets: 11
⚽ Mabao aliyoruhusu: 5
Wote wameruhusu mabao katika mechi tano tu walizocheza, jambo linalodhihirisha ubora wao katika kulinda lango.
Mchezo mkubwa unakuja: Kariakoo Derby – Machi 8
Mabingwa hawa ambao hawajafungwa watakutana Machi 8 katika Uwanja wa Benjamin Mkapa katika mchezo wa Kariakoo derby kati ya Simba SC na Yanga SC. Mchezo huu utakuwa mtihani mkubwa kwa makipa wote wawili, na mashabiki wanatarajia kuona nani atabaki kuwa nguzo imara kwa timu yao.
CHECK ALSO:
Weka maoni yako