Vituo vya Kufanyia Usaili wa TRA kwa Waliochaguliwa 2025, Majina ya Walioitwa Kwenye Usaili wa TRA 2025 | Written Interview Tarehe 29-30 Machi.
Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) ilitangaza nafasi za kazi 1,596 katika fani mbalimbali kuanzia tarehe 06 hadi 19 Februari, 2025, ambapo maombi ya kazi 135,027 yalipokelewa.
TRA imepitia kwa umakini mkubwa maombi yote yaliyopokelewa na kupata waomba kazi 112,952 waliokidhi vigezo vilivyowekwa na hivyo kustahili kuitwa kwenye usaili wa mchujo wa kuandika (Written Interview) ambao unatarajiwa kufanyika kuanzia tarehe 29 hadi 30 Machi, 2025.
Majina ya waliofanikiwa yatatangazwa kwenye tovuti ya TRA (www.tra.go.tz) tarehe 22/03/2025 na pia taarifa itatumwa moja kwa moja kwa kila muombaji kupitia barua pepe yake aliyotumia wakati wa kuomba kazi. Vilevile, tarehe, mahali, na muda wa usaili zitaonyeshwa kwenye wito huo.
Vituo vya Kufanyia Usaili wa TRA kwa Waliochaguliwa 2025

Usaili wa Mchujo wa Kuandika Utafanyika Katika Mikoa 9 Kama Ifuatavyo:
Dar es Salaam – itahusisha waombaji kutoka Dar es Salaam na Pwani.
Zanzibar – itahusisha waombaji kutoka Unguja na Pemba.
Arusha – itahusisha waombaji kutoka Arusha, Manyara, Kilimanjaro na Tanga.
Dodoma – itahusisha waombaji kutoka Morogoro, Dodoma, Singida, Iringa na Tabora.
Mtwara – itahusisha waombaji kutoka Mtwara, Lindi na Ruvuma.
Mbeya – itahusisha waombaji kutoka Mbeya, Songwe na Rukwa.
Mwanza – itahusisha waombaji kutoka Mwanza, Shinyanga, Mara na Simiyu.
Kagera – itahusisha waombaji kutoka Kagera na Geita.
Kigoma – itahusisha waombaji kutoka Kigoma na Katavi.
CHECK ALSO:
- Majina ya Walioitwa Usaili TRA 2025 Kutangazwa Rasmi Machi 22
- TRA Kutangaza Majina ya Waliochaguliwa Kwenye Usaili Leo
- Jinsi ya Kutuma Maombi Ajira Jeshi la Polisi 2025
- Nafasi za Polisi 2025 Tangazo la Ajira Jeshi la Polisi
- Nafasi za Ajira Jeshi la Polisi Tanzania 2025 Sifa, Tarehe Muhimu na Jinsi ya Kutuma Maombi
Weka maoni yako