Waamuzi wa Kimataifa wa Misri Kusimamia Mechi ya Yanga vs Simba 25 Juni 2025 | TPLB Yatangaza Waamuzi wa Kariakoo Derby: Yanga SC dhidi ya Simba SC.
Bodi ya Ligi Kuu Tanzania Bara (TPLB) imetangaza rasmi majina ya waamuzi watakaochezesha mchezo wa Kariakoo Derby kati ya Young Africans SC (Yanga) na Simba SC. Mchezo huu wa 184 wa Ligi Kuu Tanzania Bara (NBC Premier League) utachezwa Jumatano, Juni 25, 2025, kuanzia saa 11:00 Jioni kwenye Uwanja wa Benjamin Mkapa jijini Dar es Salaam.
Kwa mujibu wa taarifa ya TPLB, waamuzi wote walioteuliwa kuchezesha mechi hiyo ni Misri, jambo linalodhihirisha umuhimu mkubwa wa mechi hii.
Waamuzi wa Kimataifa wa Misri Kusimamia Mechi ya Yanga vs Simba 25 Juni 2025

Majina ya Maofisa wa Mchezo:
Mwamuzi wa Kati: Amin Mohamed Amin Omar (Misri)
Mwamuzi Msaidizi 1: Mahmoud Ahmed Abo El Regal (Misri)
Mwamuzi Msaidizi 2: Samir Gamal Saad Mohamed (Misri)
Mwamuzi wa Akiba (4th Official): Ahmed Mahrous (Misri)
Kamishna wa Mchezo: Salim Omary Singano (Tanzania)
Uteuzi wa waamuzi wa kimataifa kutoka nje ya nchi ni hatua ya kuboresha uwazi, uadilifu na uadilifu wa mchezo huu mkubwa unaovutia maelfu ya mashabiki nchini na nje ya mipaka ya Tanzania.
CHECK ALSO:
Weka maoni yako