Wachezaji wa Yanga Waondoka Uwanjani, Hatma ya Alama 3 Matatani | Kufuatia hali ya sintofahamu katika mchezo wa Kariakoo kati ya Yanga SC na Simba SC, wachezaji wa Yanga SC waliondoka kwenye Uwanja wa Benjamin Mkapa huku wengine wakitumia usafiri wao.
Wachezaji wa Yanga Waondoka Uwanjani, Hatma ya Alama 3 Matatani
Kwa mujibu wa taarifa rasmi, mechi hiyo haikuchezwa ilivyopangwa baada ya Bodi ya Ligi Kuu Tanzania (TPLB) kutangaza kuahirisha mchezo huo. Hali hii imezua maswali mengi kwa mashabiki wa soka nchini hasa kuhusiana na hatima ya pointi tatu na iwapo Yanga SC itapata ushindi kwenye jedwali.
Pointi tatu hazijatolewa
Tofauti na matarajio ya mashabiki, hakuna uamuzi wa kuipa Yanga SC pointi tatu na ushindi wa mabao matatu kwa sababu zifuatazo:
- Hakukuwa na afisa yeyote wa mchezo huo kutoka TFF au TPLB aliyekuwepo uwanjani ili kuthibitisha matokeo ya kisheria.
- Mamlaka husika zinahitaji kufanya uchunguzi wa kina kuhusu sababu za kutopigwa kwa mechi hiyo kabla ya kutoa uamuzi rasmi.
Kwa sasa ukurasa wa mechi ya Machi 8 Kariakoo Derby umefungwa rasmi na wadau wa soka wanasubiri kutangazwa tarehe mpya baada ya uchunguzi kukamilika.
CHECK ALSO:
Weka maoni yako