Walioitwa Kujiunga na Shule ya Polisi Tanzania 2025 Ajira Jeshi la Polisi, Majina ya Waliochaguliwa Kujiunga Shule ya Polisi Moshi June 2025 | Jeshi la Polisi Tanzania limetangaza rasmi majina ya vijana waliochaguliwa kujiunga na Shule ya Polisi Moshi kwa mzunguko wa Juni 2025. Tangazo hili linaelekeza hatua muhimu za kuzingatia na taratibu za kuripoti shule kwa ajili ya mafunzo ya awali.
Hii ni fursa muhimu kwa vijana wenye nia ya kujiunga na Jeshi la Polisi na kuanza maisha mapya ya taaluma ya ulinzi na usalama nchini. Katika makala haya, tutakupa mwongozo kamili kuhusu ni lini, wapi, na vipi vijana waliochaguliwa wanapaswa kuripoti Shule ya Polisi Moshi, pamoja na vifaa muhimu vinavyotakiwa kuletwa. Pia tutaelezea taratibu maalum kwa waliotokea maeneo tofauti Tanzania Bara na Zanzibar.
Walioitwa Kujiunga na Shule ya Polisi Tanzania 2025 Ajira Jeshi la Polisi
Tarehe Muhimu za Kuripoti Shule ya Polisi Moshi Juni 2025
Kwa mujibu wa tangazo rasmi la Jeshi la Polisi, vijana waliochaguliwa kujiunga na Shule ya Polisi Moshi wanatakiwa kuripoti chuoni kuanzia tarehe 12 Juni 2025 hadi 14 Juni 2025. Ni muhimu sana kuhakikisha muda huu unaheshimiwa kwani baada ya tarehe 14 Juni 2025, vijana hawatakaribishwa na watahesabiwa kujiuzulu mafunzo kwa hiari yao wenyewe.

Vijana Waliofanyiwa Usaili Dar es Salaam
Vijana waliofanyiwa usaili katika mikoa ya Dar es Salaam, hasa walioko vikosi chini ya Makao Makuu ya Polisi, wanatakiwa kuripoti saa 12:00 asubuhi tarehe 12 Juni 2025 katika uwanja wa gwaride ulioko Kambi ya Polisi, barabara ya Kilwa (nyuma ya kituo cha Polisi Kilwa Road). Hapa watapata usaidizi wa mpangilio wa safari ya kwenda Shule ya Polisi Moshi.
Vijana Waliofanyiwa Usaili Mikoa Mingine Tanzania Bara
Kwa wale waliokamilisha usaili katika mikoa mingine ya Tanzania Bara, watalazimika kuripoti kwa makamanda wa polisi wa mikoa yao walikofanyiwa usaili tarehe 11 Juni 2025 saa 2:00 asubuhi. Hii ni kwa ajili ya kupanga utaratibu wa usafiri kuelekea Shule ya Polisi Moshi.
Vijana Waliofanyiwa Usaili Zanzibar (Unguja na Pemba)
Kwa upande wa Zanzibar, vijana waliosailiwa katika visiwa vya Unguja na Pemba wanatakiwa kuripoti Makao Makuu ya Polisi Zanzibar (Ziwani) tarehe 11 Juni 2025 saa 2:00 asubuhi kwa ajili ya kupanga safari ya kwenda Moshi/Walioitwa Kujiunga na Shule ya Polisi Tanzania 2025 Ajira Jeshi la Polisi.
Vifaa Muhimu Vinavyotakiwa Kuletwa Chuoni
Jeshi la Polisi limeweka orodha ya vifaa vinavyotakiwa kuletwa na kila mwanafunzi anayeripoti Shule ya Polisi Moshi. Hii ni kuhakikisha kila mwanafunzi anajiandaa ipasavyo kwa mafunzo ya kujiendeleza kimasomo na kimichezo.
Vifaa vya Mchezo na Mazoezi
- Traki suti rangi ya buluu yenye ufito mweupe
- Fulana (t-shirt) nyeupe isiyo na maandishi
- Raba na soksi nyeusi
- Bukta mbili za buluu kwa ajili ya michezo na mazoezi
- Sanduku la chuma (tranka) la rangi ya buluu

Vifaa vya Kulala
- Chandarua cheupe cha duara (si cha pembe nne)
- Shuka za buluu mpauko (light blue), jozi mbili (shuka nne)
- Pasi ya mkaa
- Blanketi moja la kijivu lisilo na maua, si duveti
Vifaa vingine Vinavyohitajika
- Kikombe cha plastiki chenye rangi ya mfupa (cream light)
- Sahani moja ya chuma (steel dish plate)
- Vifaa vya usafi: sururu moja lenye mpini, ndoo mbili ndogo na fagio la chelewa
- Kadi ya bima ya afya (NHIF) au fedha taslimu Tsh 50,400 kwa wasio na kadi
- Vyeti halisi vya taaluma (original academic certificates)
- Cheti halisi cha kuzaliwa
- Kadi ya NIDA au namba ya utambulisho wa taifa
- Nakala 5 za kila cheti na kadi za NIDA za wazazi au watu wa karibu (kama baba, mama, babu, mjomba, shangazi n.k)
- Passport size picha 6 za rangi ya nyuma buluu
- Fedha za kujikimu chuoni
Jeshi la Polisi linasisitiza kuwa simu za mkononi haziruhusiwi kabisa kuletwa chuoni.
ANGALIA HAPA MAJINA >>> TANGAZO_LA_KURIPOTI_SHULE_YA_POLISI_MOSHI
CHECK ALSO:
Weka maoni yako