Wiliete SC Vs Yanga Leo Saa Ngapi?

Wiliete SC Vs Yanga Leo Saa Ngapi? 19/09/2025 Ligi ya Mabingwa Afrika hatua ya awali ya mtoano, Young Africans SC (Yanga SC) imewasili Angola kwa ajili ya mchezo wa mkondo wa kwanza wa Ligi ya Mabingwa Afrika 2025/26. Timu hiyo inatarajiwa kushuka dimbani Ijumaa hii kwenye Uwanja wa Estadio 11 de Novembro kumenyana na mwenyeji, Wiliete Sports Clube.

Wiliete SC Vs Yanga Leo Saa Ngapi?

Mechi hiyo itaanza saa 12:00 jioni. Kwa SAA za Afrika Mashariki, ikiwa ni hatua muhimu kwa Yanga SC katika kusaka nafasi ya kutinga hatua ya makundi ya kuwania kufuzu kwa vilabu kuu barani Afrika.

Kwa mashabiki wa Yanga, hii ni fursa nyingine ya kuiona timu yao ikijaribu kuendeleza mbio za mafanikio katika mashindano ya kimataifa. Ushindi wa ugenini unaweza kuwapa faida kubwa kuelekea mchezo wa marudiano utakaopigwa jijini Dar es Salaam.

Wiliete SC Vs Yanga Leo Saa Ngapi?
Wiliete SC Vs Yanga Leo Saa Ngapi?

Hata hivyo, Wiliete Sports Clube inasalia kuwa mpinzani mwenye rekodi kali katika ligi ya Angola, na kuifanya mechi hii kuwa na ushindani mkubwa. Yanga SC itahitaji kuonyesha nidhamu kubwa, ukomavu wa kimataifa, na kutumia uzoefu wa nyota wao ili kupata matokeo chanya.

Kwa ujumla, macho ya mashabiki wa soka barani Afrika yataelekezwa kwenye mechi hii, kwani itatoa taswira ya namna mabingwa hao wa Tanzania wanavyoanza kampeni ya Ligi ya Mabingwa msimu huu.

CHECK ALSO:

  1. Jezi Mpya ya Mtibwa Sugar 2025/26
  2. Msimamo wa Ligi Kuu NBC Tanzania 2025/2026
  3. Ratiba ya Mechi za Leo NBC Premier League
  4. Ratiba ya Yanga Ligi ya Mabingwa Afrika CAF 2025/2026