Yanga Kucheza na Rayon Sports Kwenye Rayon Day 2025

Yanga Kucheza na Rayon Sports Kwenye Rayon Day 2025: Klabu ya Rayon Sports ya Rwanda imetangaza rasmi kuwa itacheza mechi ya kirafiki dhidi ya Yanga SC ya Tanzania ikiwa ni sehemu ya Rayon Day 2025. Mchezo huo umepangwa kuchezwa Agosti 2025 kwenye Uwanja wa Amahoro mjini Kigali.

Yanga Kucheza na Rayon Sports Kwenye Rayon Day 2025

Rayon Day imekuwa desturi kwa klabu hiyo ya Rwanda, ikilenga kuwaleta mashabiki pamoja, kuipa motisha timu na kujiandaa na msimu mpya wa ligi.

Mchezo huo unatarajiwa kuvutia maelfu ya mashabiki kutoka Rwanda na Tanzania, na Yanga inatarajiwa kuwasili na kikosi chake kamili kinachojiandaa na msimu wa Ligi Kuu ya NBC, pamoja na mashindano ya kimataifa.

Yanga SC Waalikwa Namibia kwa Maandalizi ya Msimu wa Kimataifa

Mbali na mchezo huo wa kirafiki, Yanga SC pia imepata mwaliko wa kushiriki mazoezi ya maandalizi (Preseason) nchini Namibia, ambapo itashiriki mashindano maalum ya kirafiki na klabu kadhaa za Afrika.

Yanga Kucheza na Rayon Sports Kwenye Rayon Day 2025
Yanga Kucheza na Rayon Sports Kwenye Rayon Day 2025

Klabu zilizothibitishwa kushiriki na Yanga ni:

  • African Stars 🇳🇦 (Namibia – mwenyeji)
  • Petro de Luanda 🇦🇴 (Angola)
  • Lioli FC 🇱🇸 (Lesotho)

Mashindano haya yanalenga kuimarisha kiwango cha ushindani kabla ya msimu mpya wa ligi na mashindano ya CAF, na Yanga inachukua fursa hiyo kuboresha kikosi chake hasa kwa kuongeza wachezaji wapya.

CHECK ALSO:

  1. Fountain Gate Yasalia Ligi Kuu NBC 2025/26, Ushindi Dhidi ya Stand United
  2. Yanga Kushiriki Champions Tournament Nchini Namibia Agosti 2025
  3. Kennedy Musonda Ajiunga na Hapoel Ramat Gan ya Israel
  4. Ratiba Kamili ya LaLiga 2025/2026