Yanga SC Kusaka Ushindi wa Dabi 5 Mfululizo: Je, Wataisawazisha Rekodi ya Simba SC?.
Young Africans SC (Yanga SC) watakuwa dimbani katika mchezo wao wa derby dhidi ya Simba SC, kusaka ushindi utakaoiwezesha kufikia rekodi ya kushinda mechi tano mfululizo za derby, rekodi ambayo kwa sasa inashikiliwa na Simba SC.
Katika historia ya Ligi Kuu Tanzania Bara, Simba SC ndiyo klabu pekee iliyofanikiwa kushinda mechi tano mfululizo za derby kati ya 2004 na 2005, huku ikionyesha ubabe dhidi ya wapinzani wao wa jadi, Yanga SC.
Yanga SC Kusaka Ushindi wa Dabi 5 Mfululizo
Rekodi ya Ushindi wa Simba SC Dabi 5 Mfululizo
✅ 07/08/2004 – Simba SC 2-1 Yanga SC (Ulimboka Mwakingwe, Emmanuel Kisiga ⚽ | Pitchou Congo ⚽)
✅ 18/09/2004 – Simba SC 1-0 Yanga SC (Man Machuppa ⚽)
✅ 17/04/2005 – Yanga SC 1-2 Simba SC (Nurdin Msigwa ⚽ | Man Machuppa, Nyanda ⚽⚽)
✅ 02/07/2005 – Simba SC 2-0 Yanga SC (Emma Gabriel, Mussa Mgosi ⚽⚽)
✅ 21/08/2005 – Simba SC 2-0 Yanga SC (Nico Nyagawa ⚽)
Kwa sasa, Yanga SC wana rekodi ya ushindi wa dabi nne mfululizo, na ikiwa watashinda mchezo ujao dhidi ya Simba SC, watakuwa wamesawazisha rekodi hiyo ya kihistoria.

Je, Yanga SC wanaweza kuweka historia?
Mchezo ujao kati ya Yanga SC na Simba SC unatarajiwa kuwa wa kusisimua zaidi, huku mashabiki wakisubiri kuona iwapo Yanga SC itafanikiwa kufikia rekodi ya watani zao au Simba SC itazuia historia hiyo kutokea.
Mashabiki wa soka nchini Tanzania wanatarajia mechi kali na yenye ushindani kati ya timu hizi mbili kongwe. Je, Yanga SC itaweka historia au Simba SC itabaki kuwa klabu pekee yenye rekodi ya kutwaa mataji matano mfululizo?
Tusubiri tuone matokeo ya Kariakoo Derby yatakuwaje!
CHECK ALSO:
Weka maoni yako