Yanga SC Waibuka Mabingwa wa Ngao ya Jamii 2025

Yanga SC Waibuka Mabingwa wa Ngao ya Jamii 2025: Yanga SC imeendeleza ubabe katika soka la Tanzania baada ya kuifunga Simba SC bao 1-0 katika fainali ya Ngao ya Jamii 2025 Uwanja wa Benjamin Mkapa jijini Dar es Salaam. Ushindi huu unaifanya Yanga kuwa mabingwa wa Ngao ya Jamii mwaka huu na kuendeleza rekodi ya kutwaa mataji sita mfululizo kwenye Kariakoo derby.

Yanga SC Waibuka Mabingwa wa Ngao ya Jamii 2025

Kwa ushindi huo, Yanga SC mbali na kujihakikishia kuanza kwa kasi msimu huu wa Ligi Kuu Tanzania Bara, lakini pia wameendelea kudhihirisha ubabe wao katika mechi kubwa zaidi nchini, Kariakoo derby. Taji hili la sita mfululizo linaweka rekodi mpya katika mchezo huu wa jadi unaozikutanisha timu mbili kongwe na maarufu nchini.

Yanga SC Waibuka Mabingwa wa Ngao ya Jamii 2025
Yanga SC Waibuka Mabingwa wa Ngao ya Jamii 2025

Ngao ya Jamii ni mechi ya ufunguzi wa msimu huu, inawakutanisha bingwa wa Ligi Kuu ya Tanzania Bara dhidi ya mshindi wa Kombe la FA, au mshindi wa pili ikiwa bingwa wa ligi hiyo pia ametwaa kombe hilo. Mechi hii inachukuliwa kuwa mtihani wa kujiandaa na msimu mpya, na kwa mara nyingine Yanga SC walionyesha ubora wao kwa kushinda mbele ya maelfu ya mashabiki waliohudhuria uwanjani.

Ushindi huu unadhihirisha kuwa Yanga SC iko tayari kwa changamoto za msimu mpya wa 2025/2026, ikiwemo Ligi Kuu na mashindano ya kimataifa ya CAF. Kwa upande wa Simba SC, matokeo haya yanawakilisha changamoto kwa timu ya makocha kushughulikia mapungufu yao kabla ya kuanza kwa msimu rasmi.

CHECK ALSO:

  1. Young Africans Sport Club vs Simba SC Leo 16/09/2025
  2. CAF Yaifungia Simba Mechi Moja ya Nyumbani ya Ligi ya Mabingwa Afrika
  3. Rekodi za Simba na Yanga Ngao ya Jamii
  4. Kikosi cha Simba Leo vs Yanga 16/09/2025