Yanga SC Yavunja Mkataba na Kocha Mkuu Romain Folz, Patrick Mabedi Kushika Usukani kwa Muda. Bodi ya Wakurugenzi ya Young Africans Sports Club (Yanga SC) imetangaza rasmi kuvunja mkataba na kocha wa timu hiyo, Romain Folz baada ya muda wa ushirikiano.
Katika taarifa iliyotolewa na Idara ya Habari na Mawasiliano ya Yanga SC, klabu hiyo imemshukuru kocha Folz kwa mchango wake katika timu hiyo na kumtakia mafanikio katika majukumu yake ya baadaye. Bodi hiyo ilieleza kuwa uamuzi huo ni sehemu ya mabadiliko ya kiufundi ili kuimarisha kikosi kwa ajili ya mashindano yajayo.
Yanga SC Yavunja Mkataba na Kocha Mkuu Romain Folz
“Uongozi wa Young Africans SC unamshukuru kocha Romain Folz kwa mchango wake ndani ya Klabu yetu na unamtakia kila la kheri katika majukumu yake yanayofata,” ilisema sehemu ya taarifa hiyo.

Wakati harakati za kusaka kocha mpya zikiendelea, Yanga itakuwa chini ya kocha msaidizi Patrick Mabedi ambaye ataiongoza kwa muda timu hiyo. Hatua hii inalenga kuhakikisha uthabiti na mwendelezo katika programu za mafunzo na maandalizi ya mechi zijazo.
Yanga SC imekuwa miongoni mwa klabu zinazoongoza katika soka la Tanzania na Afrika Mashariki, hivyo mabadiliko hayo ya makocha yanatarajiwa kuleta athari katika mwenendo wa timu katika mashindano ya ndani na nje ya nchi.
Kwa sasa mashabiki na wadau wa soka nchini wanafuatilia kwa karibu hatua zitakazochukuliwa na uongozi wa klabu hiyo kumpata kocha mpya wa kuziba nafasi iliyoachwa wazi na Folz.
CHECK ALSO:
Weka maoni yako