Yanga SC Yazindua Kampeni ya Tofali la Ubingwa

Yanga SC Yazindua Kampeni ya Tofali la Ubingwa | Young Africans SC (Yanga SC) imezindua rasmi kampeni ya “TOFALI LA UBINGWA” leo Julai 11, 2025, ili kuwahamasisha wanachama wake kulipa ada zao na kusajili wanachama wapya, ikiwa ni sehemu ya maandalizi ya msimu ujao wa 2025/26.

Kwa mujibu wa uongozi wa Yanga SC, kampeni hii inalenga kuimarisha ushirikiano kati ya klabu na mashabiki wake, lengo kuu ikiwa ni kufikia wanachama milioni moja ndani ya muda mfupi.

Yanga SC Yazindua Kampeni ya Tofali la Ubingwa

Yanga SC Yazindua Kampeni ya Tofali la Ubingwa
Yanga SC Yazindua Kampeni ya Tofali la Ubingwa

JINSI YA KULIPIA

MFANO WA JINSI YA KULIPIA ADA YAKO YA UANACHAMA KUPITIA MTANDAO WA VODACOM (M-PESA).

1. PIGA *150*00#
2. CHAGUA 4 – LIPA KWA MPESA
3. CHAGUA 4 – WEKA NAMBA YA KAMPUNI
4. NAMBA YA KAMPUNI 888844
5. WEKA NAMBA YA KUMBUKUMBU (WEKA NAMBA YAKO YA SIMU).
6. WEKA KIASI – 24,000/= Kama ni Mwaka mmoja au 48,000 Kama ni miaka Miwili
7. KISHA WEKA NAMBA YAKO YA SIRI
8. INGIZA 1 KUKUBALI

Katika uzinduzi huo, uongozi wa Yanga SC ulieleza kuwa “Tofali la Ubingwa” si kampeni ya mtu mmoja, bali ni wito wa pamoja kwa mashabiki wa Yanga kuchangia mafanikio ya klabu hiyo, si kwa kushangilia tu bali pia kuwa sehemu ya mfumo rasmi wa klabu kupitia uanachama hai.

CHECK ALSO:

  1. Edwin Balua Asajiliwa Enosis Paralimni ya Cyprus kwa Mkopo Kutoka Simba
  2. Chelsea vs PSG Fainali ya Kombe la Dunia la Vilabu Jumapili Hii
  3. Zesco United Wamtaka Clatous Chama, Azam Pia Wanahitaji Huduma Yake
  4. Wachezaji Wanaotajwa Kuondoka Simba 2025