Yanga vs Coastal Union Kombe la Shirikisho la CRDB 12/03/2025 | Yanga SC dhidi ya Coastal Union katika hatua ya 32 bora ya Kombe la Shirikisho.
Yanga vs Coastal Union Kombe la Shirikisho la CRDB 12/03/2025
Mabingwa watetezi wa Kombe la Shirikisho, Young Africans (Yanga SC) wanakabiliwa na mtihani mgumu dhidi ya Coastal Union katika hatua ya 32 bora ya michuano hiyo mwaka huu.
Yanga SC ambao msimu uliopita walitwaa taji hili baada ya kuifunga Azam FC kwa penalti 6-5 kwenye Uwanja Mpya wa Amaan Complex visiwani Zanzibar, wanatarajia kuendeleza rekodi yao ya mafanikio katika michuano hii. Ushindi huo uliwapa ubingwa wao wa tatu mfululizo, na kuwafanya kuwa miongoni mwa timu zenye rekodi bora katika michuano hiyo.

Historia ya Mechi ya Yanga SC vs Coastal Union
Yanga SC na Coastal Union awali zilikutana katika fainali ya kombe la Shirikisho mwaka 2022 iliyovutia sana ambapo mchezo huo uliisha kwa sare ya 3-3 kabla ya Yanga kushinda kwa penati 4-1. Hii inaashiria kuwa mechi yao ya sasa inaweza kuwa na ushindani mkubwa.
Ratiba na hatua zinazofuata
Mechi za hatua ya 32 bora zimepangwa kuchezwa kati ya Machi 4 na 14, ambapo mshindi wa pambano kati ya Yanga SC na Coastal Union atatinga hatua ya 16 bora, ambapo watamenyana na Songea FC.
Mashabiki wa soka wanatarajia mchezo wa kusisimua kati ya timu hizi mbili, huku Yanga SC wakisaka taji lao la nne mfululizo katika michuano hii ya Kombe la Shirikisho.
CHECK ALSO:
Weka maoni yako