Yanga Yaibuka Bingwa CRDB Cup 2025, Yafikisha Makombe Matano Msimu Huu | Young Africans Sports Club (Yanga SC) imeweka historia kwa kutwaa taji la CRDB Cup baada ya kuifunga Singida Black Stars mabao 2-0 katika mchezo wa fainali. Ushindi huu umeiwezesha Yanga kutwaa mataji matano ndani ya msimu mmoja, msimu wa 2024/2025.
Yanga Yaibuka Bingwa CRDB Cup 2025, Yafikisha Makombe Matano Msimu Huu
Yanga SC tayari ilikuwa imeshatwaa makombe yafuatayo kabla ya CRDB Cup:
- Toyota Cup
- Muungano Cup
- Ngao ya Jamii (Community Shield)
- Kombe la NBC Premier League (NBCPL)
Kwa ushindi huo Yanga SC imethibitisha kutawala kwa soka la Tanzania msimu huu na kudhihirisha ubora wa kikosi chake na makocha.
Kwa mashabiki na wanachama wa Yanga ushindi huu ni wa mafanikio makubwa, lakini ni lazima uongozi wa klabu hiyo uendelee kuwekeza kwa kiasi kikubwa ili kuendeleza mafanikio haya msimu ujao hasa katika mashindano ya kimataifa.
CHECK ALSO:
Weka maoni yako