YANGA Yarejea na Kikosi Kamili, Nyota Wanne Wafanya Mazoezi | Klabu ya Yanga imepata habari njema baada ya wachezaji wake wanne tegemeo kurejea mazoezini baada ya kupona majeraha, huku nahodha msaidizi wa timu hiyo, Dickson Job akithibitisha kuwa jeraha lake la goti linaendelea vizuri.
YANGA Yarejea na Kikosi Kamili, Nyota Wanne Wafanya Mazoezi
Job aliumia katika mechi ya Ligi Kuu Bara dhidi ya Namungo, ambapo Yanga ilishinda mabao 2-0 ugenini. Dakika ya 82 alitolewa nje na nafasi yake kuchukuliwa na Jonas Mkude. Akizungumzia hali yake, Ayubu alisema:
“Ninaendelea vizuri kwa sasa kwa sababu nilikuwa na jeraha kidogo la goti.”
Mchezaji huyo amekuwa nguzo ya safu ya ulinzi ya Yanga, hivyo kurejea kwake kunaendelea kuwa na umuhimu mkubwa kwa timu hiyo.
Nyota Wanne Warudi Mazoezini
Wakati hali ya Job ikileta matumaini, nyota wanne wa Yanga—Khalid Aucho, Clement Mzize, Chadrack Boka, Aziz Andambwile—wameanza mazoezi baada ya kuwa nje kwa muda kutokana na majeraha.
Wachezaji hao walikosekana kwenye mchezo wa CAF Champions League hatua ya makundi dhidi ya Al Hilal ambapo Yanga ilifungwa mabao 2-0 nyumbani, na pia hawakushiriki katika ushindi wa mabao 2-0 dhidi ya Namungo. Kurejea kwao kunatoa ahueni kwa kikosi hicho wanapojiandaa kwa mechi muhimu zinazokuja.
Mashabiki wa Yanga wanatarajia kuona nguvu mpya kwenye kikosi chao huku msimu wa michuano mikubwa ukiendelea kushika kasi.
ANGALIA PIA:
Weka maoni yako