Yanga Yatoa Mapumzika ya Kikosi chake, Wachezaji Kurejea Mazoezini Juni 1

Yanga Yatoa Mapumzika ya Kikosi chake, Wachezaji Kurejea Mazoezini Juni 1: Baada ya Mchezo wa Kirafiki na Singida Black Stars.

Yanga Yatoa Mapumzika ya Kikosi chake, Wachezaji Kurejea Mazoezini Juni 1

Timu ya Young Africans Sports Club (Yanga SC) ikiwa imepumzishwa rasmi baada ya kushiriki mchezo wa kirafiki dhidi ya Singida Black Stars uliochezwa hivi karibuni.

Mchezo huo ulikuwa ni sehemu ya maandalizi ya timu hiyo kuelekea mechi zilizosalia za Ligi Kuu Tanzania Bara, pamoja na fainali ya Kombe la CRDB.

Yanga Yatoa Mapumzika ya Kikosi chake, Wachezaji Kurejea Mazoezini Juni 1

Kwa mujibu wa taarifa ya ndani ya klabu, wachezaji ambao hawajaitwa na timu zao za taifa watatumia kipindi hiki kupumzika kabla ya kurejea kambini Juni 1, 2025. Hatua hii inalenga kuwapa muda wa kupumzika na kurejesha nguvu baada ya msimu mrefu wa ushindani.

Wachezaji waliochaguliwa kujiunga na timu zao za taifa wataendelea na majukumu yao ya kimataifa kama kawaida. Hata hivyo, kwa waliobaki, makocha wamepanga kuanza tena mazoezi mapema Juni ili kujiandaa na hatua za mwisho za mashindano ya ndani, hasa mechi za mwisho za Ligi Kuu na fainali ya Kombe la CRDB.

CHECK ALSO: