Zesco United Wamtaka Clatous Chama, Azam Pia Wanahitaji Huduma Yake: Klabu ya Zesco United ya Zambia imewasilisha ofa rasmi kwa kiungo mkongwe Clatous Chama (34) baada ya kuachana na klabu ya Tanzania ya Young Africans SC (Yanga).
Kwa mujibu wa vyanzo vya ndani, tayari mazungumzo kati ya Chama na Zesco yameanza, na kiungo huyo ameahirisha mpango wake wa kujiunga na klabu moja ya Kiarabu ili kutoa nafasi kwa ofa mpya.
Zesco United Wamtaka Clatous Chama, Azam Pia Wanahitaji Huduma Yake

Timu zinazowania saini ya Chama kwa sasa ni:
- Zesco United (Zambia)
- Azam FC (Tanzania)
Raia wa Zambia, Clatous Chama ni miongoni mwa viungo waliong’ara kwenye Ligi Kuu Tanzania Bara akiwa na Simba SC, kabla ya kujiunga na RS Berkane (Morocco), kurejea Simba, kisha kusajiliwa Yanga kwa muda mfupi msimu wa 2023/24.
Ingawa awali Chama alikuwa tayari kujiunga na klabu ya Mashariki ya Kati, mambo yamebadilika tangu alipovutiwa na ofa kutoka kwa klabu hizi mbili zinazomfahamu vyema na zinahitaji huduma yake kwa haraka.
CHECK ALSO:






Weka maoni yako