Chelsea Yaibuka na Ushindi, Palmer Akosa Penalti ya Kwanza | Chelsea walipata ushindi mwembamba wa bao 1-0 dhidi ya Leicester City kwenye Uwanja wa Stamford Bridge, huku beki Marc Cucurella akifunga bao pekee la ushindi dakika ya 60.
Chelsea Yaibuka na Ushindi, Palmer Akosa Penalti ya Kwanza
Hata hivyo, mshangao mkubwa kwa wengi ni kwamba Cole Palmer alikosa penalti kwa mara ya kwanza katika maisha yake ya soka. Palmer, ambaye ana rekodi kubwa ya kupiga penalti, alishindwa kumwokoa mlinda mlango wa Leicester, kitu ambacho mashabiki wa The Blues hawakutarajia.
Tottenham sare vikali dhidi ya Bournemouth
Katika mechi nyingine ya kusisimua, Tottenham Hotspur na Bournemouth zilitoka sare ya 2-2 kwenye Uwanja wa Tottenham Hotspur.
Bournemouth walikuwa wa kwanza kupata bao kupitia kwa Tavernier dakika ya 42, kabla ya Evanilson kuongeza bao la pili dakika ya 65. Tottenham ilirejesha matumaini kwa bao la Sarr dakika ya 67 na Son Heung-min akasawazisha dakika ya 84 na kuwapa Spurs pointi moja nyumbani.
Matokeo haya yanawafanya Chelsea wasonge mbele kwa ushindi huo muhimu, huku Spurs wakilazimika kujipanga upya baada ya kukosa nafasi ya kushinda mechi hiyo.
CHECK ALSO:
Weka maoni yako