Kikosi cha Pamba Jiji Chapata Ajali Dodoma

Kikosi cha Pamba Jiji Chapata Ajali Dodoma, Wilayani Bahi | Timu ya Pamba Jiji imethibitisha kuwa kikosi chake kimepata ajali leo saa 11:00 alfajiri kikiwa safarini kutoka Bukoba, Kagera kuelekea Morogoro kwa ajili ya mchezo wa Kombe la Shirikisho la CRDB dhidi ya Kiluvya United.

Kikosi cha Pamba Jiji Chapata Ajali Dodoma

Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na klabu hiyo, ajali hiyo ilitokea katika Wilaya ya Bahi, mkoani Dodoma baada ya basi la timu hiyo kugongwa na lori aina ya semi-trailer mali ya Kampuni ya Mwanza Huduma. Tukio hilo limezua taharuki kwa wachezaji hao huku baadhi yao wakiripotiwa kujeruhiwa.

Kikosi cha Pamba Jiji Chapata Ajali Dodoma

Pamba Jiji imeeleza kuwa taarifa za kiusalama zinaendelea kufuatiliwa na itaendelea kutoa taarifa zaidi kuhusu hali za wachezaji na benchi la ufundi.

Mashabiki wa soka na wanaopenda mchezo huo wanasubiri taarifa rasmi kuhusu hali za majeruhi hao na iwapo ajali hiyo itaathiri maandalizi ya timu hiyo kuelekea mchezo wao wa Kombe la Shirikisho la CRDB dhidi ya Kiluvya United unaotarajiwa kufanyika Machi 11, 2025.

CHECK ALSO: