Mwana FA Mgeni Rasmi Uzinduzi wa Uwanja wa Airtel Singida Black Stars vs Yanga Machi 24 | Naibu Waziri wa Utamaduni Sanaa na Michezo Mheshimiwa Hamis Mwinjuma maarufu kwa jina la Mwana FA ndiye atakuwa mgeni rasmi katika uzinduzi wa Uwanja wa Airtel unaomilikiwa na klabu ya Singida Black Stars.
Mwana FA Mgeni Rasmi Uzinduzi wa Uwanja wa Airtel Singida Black Stars vs Yanga Machi 24
Uzinduzi huu utafanyika Machi 24, 2025, na utakwenda sambamba na mechi kubwa kati ya Singida Black Stars na Yanga SC.

Timu zote mbili, Singida Black Stars na Yanga SC, zinatarajiwa kuingia kambini leo Machi 19, kujiandaa na mechi hiyo muhimu.
Uwanja wa Airtel unatajwa kuwa miongoni mwa viwanja vya kisasa nchini Tanzania na unatarajiwa kuboresha mazingira ya soka la ndani na kuinua hadhi ya Singida Black Stars.
MASHABIKI wa soka kote nchini wanatarajia mechi kali huku Yanga SC wakijiandaa kuonyesha ubabe wao dhidi ya wenyeji, Singida Black Stars.
Tutaendelea kukupa taarifa zaidi kuhusu maandalizi ya mechi hii na hotuba ya FA kwenye hafla ya uzinduzi. Endelea kufuatilia kwa maelezo zaidi!
CHECK ALSO:
Weka maoni yako