Mechi ya Singida Black Stars na Yanga Yasitishwa Kwa Sababu ya Mvua Kubwa | Mchezo kati ya Singida Black Stars na Yanga SC ulisitishwa kutokana na hali mbaya ya hewa iliyohusisha mvua kubwa na upepo mkali.
Mechi ya Singida Black Stars na Yanga Yasitishwa Kwa Sababu ya Mvua Kubwa
Mechi hiyo ilisimama kwa muda, ikisubiri hali ya hewa kuimarika, lakini haikurejea katika hali ya kawaida, hali iliyowalazimu waamuzi kusimamisha mchezo rasmi.

Kabla ya mechi hiyo kusimama, Singida Black Stars walikuwa wameshasawazisha bao lililofungwa na mchezaji wao Tchakei dakika ya 56. Bao hilo lilipatikana mara baada ya bao la awali la Yanga SC, lililofungwa na Ikangalombo dakika ya 17 kipindi cha kwanza. Hadi mechi hiyo inasitishwa, matokeo yalikuwa sare ya 1-1.
Meneja Walter Harson baada ya Mchezo wetu dhidi ya Singida Black Stars kushindwa kuendelea.#timuyawananchi#daimambelenyumamwiko pic.twitter.com/UyXzQrQB1L
— Young Africans SC (@YoungAfricansSC) March 24, 2025
Hadi sasa mamlaka husika haijatoa taarifa rasmi kuhusu lini na wapi mechi hiyo itaendelea au kuchezwa tena. Mashabiki wa pande zote wanasubiri tangazo kutoka kwa bodi ya ligi kuhusu mustakabali wa mchezo huo.
CHECK ALSO:
Weka maoni yako