Timu Zilizofuzu Robo Fainali ya Kombe la Shirikisho CRDB Bank 2025 | MICHUANO ya Kombe la Shirikisho Bara la Benki ya CRDB inaendelea kushika kasi, ambapo sasa hatua ya 16 bora imekamilika na timu kadhaa zimefanikiwa kutinga hatua ya robo fainali. Mashindano haya yanatoa fursa kwa vilabu kutoka ligi mbalimbali nchini kuonyesha umahiri wao na kuwania taji hilo muhimu.
Katika hatua hiyo ya mtoano, Stand United inayoshiriki Ligi Daraja la Kwanza (Ubingwa) ilifanikiwa kutinga kwenye michuano hiyo baada ya kuibuka na ushindi wa mabao 3-1 dhidi ya Giraffe Academy. Kwa ushindi huo Stand United inaungana na timu tatu za JKT Tanzania, Singida Black Stars na Mbeya City kufuzu kwa robo fainali.
Wakati michuano hiyo ikiendelea, mashabiki wa soka wanatarajia kuwepo kwa ushindani mkali katika hatua ya robo fainali, huku kila timu ikipambana kuendelea na hatua ya nusu fainali na hatimaye kutwaa ubingwa wa Kombe la Shirikisho la Bara la Benki ya CRDB Tanzania.

Timu Zilizofuzu Robo Fainali ya Kombe la Shirikisho CRDB Bank 2025
Baada ya mechi za hatua ya 16 bora, timu nne tayari zimefanikiwa kutinga hatua ya robo fainali ya michuano ya Kombe la Shirikisho Bara la Benki ya CRDB Tanzania.
- Yanga SC
- Simba SC
- JKT Tanzania
- Singida Black Stars
- Mbeya City
- Stendi United
- Kagera Sugar
- Pamba Jiji
Timu ya Stand United inayoshiriki michuano hiyo imeweka historia ya kufuzu kwa robo fainali baada ya ushindi wa mabao 3-1 dhidi ya Giraffe Academy. Timu nyingine zinaendelea kuchuana kuwania nafasi ya kufuzu katika hatua hii ya mtoano, huku mashabiki wakisubiri kuona ni timu gani zitakamilisha msururu wa robo fainali.
Michuano hiyo inaendelea kushika kasi, huku kila timu ikiwania nafasi ya kutwaa Kombe la Shirikisho la Bara la Benki ya CRDB Tanzania 2024/Timu Zilizofuzu Robo Fainali ya Kombe la Shirikisho CRDB Bank 2025.
CHECK ALSO:
Weka maoni yako