Mbeya City Yashindi Dhidi ya Stand United 2-0, Kupanda Ligi Kuu: Mbeya City imejiweka katika mazingira mazuri ya kupanda Ligi Kuu Tanzania Bara baada ya kupata ushindi wa mabao 2-0 dhidi ya Stand United katika mchezo wa michuano hiyo uliomalizika leo.
Ushindi huu unaifanya Mbeya City kushika nafasi ya pili kwenye msimamo wa ligi hiyo ikiwa na matumaini makubwa ya kupanda moja kwa moja.
Mbeya City Yashindi Dhidi ya Stand United 2-0, Kupanda Ligi Kuu
⚽ Mbeya City 2-0 Stand United
✅ 17’ Willy
✅ 45’ Eliud
Kwa ushindi huo, Mbeya City inafikisha pointi 55, pointi tano mbele ya vinara Mtibwa Sugar, wenye pointi 60. Stand United iliyokuwa ikiwania nafasi ya kwanza, sasa ina pointi 52 na kubaki nafasi ya tatu.

Msimamo wa Championship (Top 4) Baada ya Mechi
1️⃣ Mtibwa Sugar – Mechi 25, Alama 60
2️⃣ Mbeya City – Mechi 25, Alama 55
3️⃣ Stand United – Mechi 25, Alama 52
4️⃣ Geita Gold – Mechi 25, Alama 51
Msimamo wa Ligi na Hatma ya Timu
Nafasi ya 1 & 2: Zitaingia moja kwa moja Ligi Kuu Tanzania Bara msimu ujao.
Nafasi ya 3 & 4: Zitacheza Playoff, ambapo mshindi atakutana na timu ya mkiani kutoka Ligi Kuu. Mshindi wa mwisho atapata nafasi ya kucheza Ligi Kuu msimu ujao.
Huku kila timu ikiwa imebakiwa na mechi tano pekee kabla ya msimu huu kumalizika, mchuano utaendelea kuwa mkali, hasa kwa timu za Mbeya City, Stand United, na Geita Gold zote zikiwania nafasi ya kupanda au kufuzu.
Je, Mbeya City inaweza kumaliza nafasi mbili za juu na kurejea Ligi Kuu moja kwa moja? Mashabiki wanasubiri kwa hamu hatma ya msimu huu wa Championship!
CHECK ALSO:
Weka maoni yako