Barcelona na PSG Zatinga Nusu Fainali UEFA 2025

Barcelona na PSG Zatinga Nusu Fainali UEFA 2025 | Barcelona na PSG zitatinga nusu fainali ya Ligi ya Mabingwa 2024/2025.

Barcelona na PSG Zatinga Nusu Fainali UEFA 2025

Vilabu vya Uhispania Barcelona na Paris Saint-Germain (PSG) vimefuzu kwa nusu fainali ya UEFA Champions League 2024/2025, licha ya kupoteza mechi zao za mkondo wa pili.

Barcelona imesonga mbele kwa ushindi wa jumla ya mabao 5-3 dhidi ya Borussia Dortmund ya Ujerumani, huku PSG ikisonga mbele kwa ushindi wa jumla ya mabao 5-4 dhidi ya Aston Villa ya Uingereza.

Katika mchezo wa mkondo wa pili uliopigwa nchini Ujerumani, Borussia Dortmund iliibuka na ushindi wa mabao 3-1 dhidi ya Barcelona. Mfungaji bora wa Dortmund, Serhou Guirassy wa Guinea, aling’ara, akifunga mabao yote matatu (hat trick) dakika ya 11, penalti, 49 na 76. Hata hivyo Barcelona walifanikiwa kutinga hatua ya 16 bora baada ya kufunga bao kupitia kwa Ramy Bensebaini wa Dortmund aliyejifunga dakika ya 54.

Barcelona na PSG Zatinga Nusu Fainali UEFA 2025
Barcelona na PSG Zatinga Nusu Fainali UEFA 2025

Kwa upande mwingine, Aston Villa ilijibu vikali dhidi ya PSG, na kuibuka washindi 3-2 katika mkondo wa pili. Villa walifunga kupitia kwa Youri Tielemans (34′), John McGinn (55′), na Ezri Konsa (57′). PSG walifunga kupitia kwa Achraf Hakimi (11′) na Nuno Mendes (28′).

Licha ya juhudi za Dortmund na Aston Villa katika mkondo wa pili, hazikutosha kutinga nusu fainali kutokana na tofauti ya mabao ya nyumbani na ugenini.

CHECK ALSO: