Yanga Yamuweka Mezani Ofa Nono Fei Toto Kuziba Pengo la Aziz Ki | Klabu ya Yanga SC imeanza rasmi mchakato wa kumrejesha kikosini kiungo Feisal Salum “Fei Toto” ili kufidia kukosekana kwa aliyekuwa nyota wake Stéphane Aziz Ki. Hatua hii imekuja baada ya klabu hiyo kufanikiwa kutatua mgogoro uliokuwepo kati yao na mchezaji huyo tangu atue Azam FC.
Habari za uhakika, Yanga SC imemjaribu Fei Toto kwa ofa kubwa ambayo ni pamoja na dau la usajili la shilingi milioni 800, pamoja na mshahara wa shilingi milioni 40 kwa mwezi, kiasi ambacho Azam FC imekuwa ikimuandalia kama sehemu ya mkataba mpya wanaotaka asaini.
Fei Toto kwa sasa analipwa mshahara wa shilingi milioni 23.5 kwa mwezi kutoka kwa Azam FC, lakini baada ya kukatwa kodi, ni shilingi milioni 15 pekee huingia kwenye akaunti yake binafsi. Mkataba wake wa sasa ni sawa na ada ya kusaini ya shilingi milioni 390.
Yanga Yamuweka Mezani Ofa Nono Fei Toto Kuziba Pengo la Aziz Ki

Vitu Maalum Vya Ziada Katika Ofa ya Yanga:
- Kujengewa nyumba ya kisasa eneo atakalopenda
- Kukabidhiwa gari la kifahari
- Hakutakiwa kushughulika na mazungumzo ya kumaliza mkataba wake na Azam FC – Yanga imesema wao watafanya kila kitu kwa niaba yake
Yanga SC imeweka wazi kuwa Fei Toto akikubali kurejea Jangwani haitafanyika kwa unyonge. Kauli yao ilisisitiza kuwa “hakuna tena masuala ya sukari,” ishara ya kujitolea kwao kumpa mchezaji huyo huduma ya hali ya juu.
CHECK ALSO:
Weka maoni yako