Ratiba NBC Premier League 2024/2025 na CRDB Federation Cup Mei na Juni: Bodi ya Ligi Tanzania (TPLB) imetoa ratiba rasmi ya mechi za mwisho za Ligi Kuu ya NBC msimu wa 2024/2025, pamoja na ratiba ya hatua za mwisho za Kombe la Shirikisho la CRDB.
Ratiba NBC Premier League 2024/2025 na CRDB Federation Cup Mei na Juni
Ratiba, iliyotolewa Mei 6, 2025, inaonyesha mwelekeo ambao msimu utakamilika kuanzia Mei hadi Juni 2025.

Mechi Muhimu za NBC Premier League
Raundi ya 26 hadi 30:
Raundi ya 26 ilianza rasmi Mei 11, 2025 kwa mchezo kati ya KMC FC na Simba SC.
Mzunguko wa 28 utafungwa Mei 28, 2025 kwa mchezo kati ya Simba SC na Singida Big Stars.
Kariakoo Derby kati ya Yanga SC na Simba SC ni mchezo wa raundi ya 29 uliopangwa kufanyika:
Tarehe: Jumapili, Juni 15, 2025
Muda: Saa 11:00 jioni
Uwanja: Benjamin Mkapa, Dar es Salaam
Mzunguko wa Mwisho (R30):
Utaanza Jumapili, Juni 22, 2025 ukihusisha michezo yote ya mwisho, ikiwemo:
Yanga SC vs Dodoma Jiji
Coastal Union vs Tabora United
Fountain Gate vs Azam FC
CRDB Bank Federation Cup
Nusu Fainali:
Semi Fainali ya Kwanza: Mei 18, 2025
Semi Fainali ya Pili: Mei 31, 2025
Fainali:
Itapigwa kati ya tarehe 26–28 Juni 2025
Mapumziko ya FIFA (International Break)
Tarehe: 2 hadi 10 Juni 2025
Kipindi hiki hakutakuwa na mechi yoyote ya ligi wala ya kombe, kupisha kalenda ya FIFA.
Mechi za Mchujo (Playoff)
Mchezo wa mchujo wa kuamua timu za kupanda au kushuka daraja utafanyika:
Leg 1 & 2: Julai 25–29, 2025 (PL vs PL)
Leg 1 & 2: Julai 3–7, 2025 (PL vs CL)
Tuzo za TFF (TFF Awards)
Tuzo za msimu wa 2024/25 zitatolewa baada ya kumalizika kwa mashindano yote. Tarehe kamili itatangazwa baadaye.
Ratiba hii inaonyesha misimu ya Ligi Kuu ya NBC na Kombe la Shirikisho la CRDB ikiingia hatua ya fainali yenye ushindani mkali. Mashabiki wanashauriwa kufuatilia kwa karibu ratiba hizi na kuhudhuria mechi kwa nidhamu ili kuepusha usumbufu. Pia ni fursa kwa vilabu kuonyesha uwezo wao kabla ya msimu kufungwa rasmi mwishoni mwa Juni.
CHECK ALSO:
Weka maoni yako