Yanga Wapo Tayari Kukosa Ubingwa wa NBC Ila Sikucheza Derby: Klabu ya Young Africans Sports Club (Yanga SC) imetoa msimamo thabiti kuelekea mwisho wa msimu wa Ligi Kuu ya NBC wa 2024/2025.
Uongozi wa klabu hiyo umesema upo tayari kunyang’anywa ubingwa wa ligi ikibidi endapo uamuzi wa kutocheza mchezo wa watani wa jadi (maarufu Kariakoo derby dhidi ya Simba SC) utawafanya wapokwe pointi 15.
Kwa mujibu wa taarifa rasmi na maandalizi ya klabu, Yanga SC imeelekeza nguvu zake kwenye mashindano ya Kombe la Shirikisho la Benki ya CRDB. Lengo kuu ni kutwaa kombe litakalowapa tiketi ya kushiriki Kombe la Shirikisho Afrika msimu ujao wa 2025/2026.
Yanga Wapo Tayari Kukosa Ubingwa wa NBC Ila Sikucheza Derby

Iwapo Yanga SC haitashiriki mechi ya Kariakoo Derby dhidi ya Simba SC inayotarajiwa kuchezwa Juni 15, 2025, Uwanja wa Benjamin Mkapa saa 11:00 jioni, inaweza kukumbana na adhabu ya pointi 15 kwa mujibu wa kanuni za TFF.
Hili linaweza kuathiri kwa kiasi kikubwa nafasi yao kwenye jedwali la ligi, lakini kwa mujibu wa taarifa yao, haitakuwa kipaumbele endapo itakinzana na maslahi yao kwenye Kombe la CRDB.
CHECK ALSO:
Weka maoni yako