Manchester City Kumsajili Rayan Cherki wa Lyon na Tijani Reijnenders wa AC Milan

Manchester City Kumsajili Rayan Cherki wa Lyon na Tijani Reijnenders wa AC Milan | Manchester City imeendeleza juhudi za kuimarisha kikosi chake kabla ya msimu mpya, na kufikia makubaliano ya awali na kiungo mshambuliaji wa Olympique Lyonnais, Rayan Cherki na pia imekamilisha dili la kumsajili kiungo wa AC Milan, Tijani Reijnenders, raia wa Uholanzi.

Manchester City Kumsajili Rayan Cherki wa Lyon na Tijani Reijnenders wa AC Milan

Kwa mujibu wa habari zilizopo, Manchester City inajiandaa kuwasilisha ofa rasmi kwa Lyon ili kukamilisha uhamisho wa Cherki, ambaye amedhamiria kuondoka kabla ya kumalizika kwa mkataba wake Juni 2026. Lyon imeeleza nia yake ya kumuuza mchezaji huyo katika dirisha hili la usajili ili kuepuka hatari ya kumpoteza bure siku zijazo.

Manchester City Kumsajili Rayan Cherki wa Lyon na Tijani Reijnenders wa AC Milan
Manchester City Kumsajili Rayan Cherki wa Lyon na Tijani Reijnenders wa AC Milan

Zaidi ya hayo, City imekamilisha makubaliano na AC Milan kwa uhamisho wa Tijani Reijnenders, ambaye anatarajiwa kuimarisha safu yake ya kiungo kabla ya msimu ujao.

Beki wa kushoto wa Wolves, Rayan Ait Nouri pia anaripotiwa kuhusishwa na kuhamia Etihad Stadium, hatua inayodhihirisha dhamira ya City kuimarisha maeneo yote ya kikosi chao.

CHECK ALSO: