Azam Yarudia Dili La Kumsajili Manula Kutoka Simba

Azam Yarudia Dili La Kumsajili Manula Kutoka Simba | Aishi Manula Kuwasili Azam FC Tena Baada ya Miaka 9. Klabu ya Azam FC imeanza tena mazungumzo ya kutaka kumsajili golikipa Mtanzania Aishi Manula baada ya kushindwa kupata nafasi katika dirisha dogo la usajili lililopita.

Azam Yarudia Dili La Kumsajili Manula Kutoka Simba

Katika majaribio ya awali, Azam FC ilimtafuta Manula kwa mkopo kutoka Simba SC, lakini dili hilo lilishindikana.

Klabu ya Azam FC imeonyesha nia ya dhati ya kutaka kumrejesha Manula ambaye aliwahi kuichezea klabu hiyo kabla ya kujiunga na Simba SC mwaka 2017. Endapo dili hilo litakamilika itakuwa ni alama ya Manula kurejea Azam Complex baada ya takribani miaka tisa.

Azam Yarudia Dili La Kumsajili Manula Kutoka Simba

Aishi Manula alianzia Azam FC kabla ya kuhamia Simba SC, ambako amekuwa mchezaji muhimu katika mafanikio ya klabu hiyo kwa takribani miaka minane. Uzoefu wake na kipa wake bora umeifanya Azam FC kuonesha nia mpya ya kumtaka ili kuimarisha safu yake ya ulinzi kwa msimu ujao.

Hali ya mazungumzo:

Kwa mujibu wa taarifa zilizo karibu na klabu hiyo, Azam FC ipo katika hatua za mwisho za mazungumzo na Simba SC na makubaliano yanatarajiwa kufikiwa kabla ya kufungwa kwa dirisha la usajili.

CHECK ALSO: