Matokeo ya Taifa Stars vs Madagascar Leo COSAFA 07/06/2025, Taifa Stars dhidi ya Madagascar: Ratiba, Uwanja na Maandalizi
Taifa Stars kumenyana na Madagascar leo kwenye michuano ya COSAFA 2025
Timu ya Taifa ya Tanzania maarufu Taifa Stars inatarajiwa kushuka dimbani leo Juni 7, 2025 kuvaana na timu ya Taifa ya Madagascar katika moja ya mechi za hatua ya makundi ya michuano ya COSAFA 2025 inayofanyika nchini Afrika Kusini.
Mechi hii ni sehemu ya jitihada za Tanzania kuimarisha nafasi yake katika mashindano ya ukanda wa Kusini mwa Afrika (COSAFA), ambapo inashiriki tena kama mgeni. Taifa Stars imekuwa katika maandalizi ya kina chini ya uelekezi wa kiufundi, hivyo kuahidi ushindani wa hali ya juu na mechi ya kusisimua kwa mashabiki wa soka ndani na nje ya Tanzania.
Mechi hii itachezwa kwenye Uwanja wa Nelson Mandela Bay mjini Gqeberha, Afrika Kusini, saa 10:00 Jioni kwa saa za Afrika Mashariki (EAT). Mashabiki wa soka nchini Tanzania wanatarajiwa kufuatilia kwa karibu mechi hii kupitia matangazo ya moja kwa moja kwenye televisheni za michezo na majukwaa ya kidijitali.
Matokeo ya Taifa Stars vs Madagascar Leo COSAFA 07/06/2025
LIVE | TANZANIA 0-0 MADAGASCAR

mchezo utaaza saa 10 kamili jioni
Mechi ya leo kati ya Taifa Stars na Madagascar ni muhimu kwa Tanzania kuanza safari ya COSAFA 2025. Mashabiki wote wa soka wanahimizwa kuiunga mkono timu ya taifa ili kuhakikisha inafanikiwa katika mashindano haya ya kimataifa.
CHECK ALSO:
Weka maoni yako