TPLB Yasema Mechi ya Kariakoo Derby Juni 15 Itaendelea Kama Ilivyopangwa | Bodi ya Ligi Kuu Tanzania Bara (TPLB) imethibitisha kuwa mechi ya watani wa jadi maarufu kama Kariakoo Derby iliyopangwa kufanyika Juni 15, 2025, hipo palepale licha ya msimamo wa Yanga SC kugomea mchezo huo hadi pale matakwa yao yatakapotekelezwa.
Mkurugenzi Mtendaji wa Bodi ya Ligi, Almasi Kasongo amesema madai yaliyotolewa na Yanga SC hayawezi kutekelezwa mara moja kwani yanahitaji mchakato mrefu na maamuzi ya kitaasisi.
TPLB Yasema Mechi ya Kariakoo Derby Juni 15 Itaendelea Kama Ilivyopangwa
“Mechi ya Juni 15 ipo palepale, maana hayo matakwa yao manne si rahisi kama inavyotajwa. Huo si mchakato wa siku moja. Mfano, wanataka Bodi ya Ligi iwe chombo huru na kijitegemee – hilo haliwezi kufanyika kwa siku moja,” alisema Kasongo.
Ameeleza kuwa kikao kilichofanyika kati ya Bodi ya Ligi na klabu hiyo ni sehemu ya utaratibu wa kawaida wa kuwasiliana na vilabu vinavyoshiriki ligi, kwani Bodi hiyo ni chombo kinachoundwa na vilabu vyenyewe.

“Ni utaratibu wa kawaida kukutana na vilabu. Bodi ya Ligi ni chombo cha vilabu. Baada ya kuahirishwa kwa mchezo wa Dabi uliopangwa Machi 08, tulipokea malalamiko kutoka kwa Yanga SC wakitaka kupewa alama tatu,” aliongeza Kasongo.
Kasongo alieleza kuwa katika kikao hicho, Young Africans SC waliwasilisha rasmi matakwa manne, ambayo ni:
Matakwa ya Yanga SC:
- Kamati ya Uendeshaji wa Bodi ya Ligi ivunjwe ndani ya saa 72
- Afisa Mtendaji Mkuu wa Bodi ya Ligi ajiuzulu
- Katibu Mkuu wa Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) ajiuzulu
- Bodi ya Ligi iwe chombo huru na kijitegemea
Hata hivyo, TPLB imesisitiza kuwa mchakato wa kushughulikia masuala ya muundo wa taasisi na maamuzi ya uongozi hauwezi kutekelezwa kwa haraka hivyo, na kwamba pambano hilo litaendelea kama ilivyopangwa/TPLB Yasema Mechi ya Kariakoo Derby Juni 15 Itaendelea Kama Ilivyopangwa.
CHECK ALSO:
Weka maoni yako