FIFA Yatuma Maafisa Tanzania Kufuatilia Migogoro ya TFF

FIFA Yatuma Maafisa Tanzania Kufuatilia Migogoro ya TFF na Uchaguzi Mkuu wa Agosti 2025 | FIFA Yaichunguza TFF: Migogoro ya Uongozi na Uchaguzi Mkuu wa Tathmini.

FIFA Yatuma Maafisa Tanzania Kufuatilia Migogoro ya TFF

Shirikisho la Mpira wa Miguu Duniani (FIFA) limethibitisha rasmi kupeleka maofisa wake nchini Tanzania kufanya uchunguzi maalum wa Shirikisho la Soka Tanzania (TFF). Hatua hii inafuatia ripoti za migogoro ya uongozi na kuingiliwa katika maamuzi ambayo yanaonekana kutishia misingi ya utawala huru wa vyama vya soka duniani kote.

Kwa mujibu wa barua iliyotumwa kwa TFF, FIFA ilisisitiza kuwa wataalamu wake watawasili nchini hivi karibuni kwa ajili ya kufanya tathimini ya kina ya hali ya uongozi ndani ya shirikisho hilo pamoja na mazingira ya maandalizi ya Uchaguzi Mkuu wa TFF unaotarajiwa kufanyika Agosti 2025.

FIFA imeweka wazi kuwa uamuzi wake wa kuingilia kati unatokana na wajibu wake wa kulinda uhuru na uadilifu wa vyama vya soka vya kitaifa kwa mujibu wa Ibara ya 14(1)(a) na 19 ya Katiba ya FIFA. Kifungu hiki kinataka kila chama mwanachama kufanya shughuli zake bila ushawishi wa nje na inaruhusu FIFA kuchukua hatua za ukaguzi au uchunguzi ikiwa kuna dalili za ukiukwaji wa kanuni hizi.

FIFA Yatuma Maafisa Tanzania Kufuatilia Migogoro ya TFF
FIFA Yatuma Maafisa Tanzania Kufuatilia Migogoro ya TFF

“Shirikisho la mpira wa miguu la taifa lazima lionyeshe uhuru wa kiutawala na kuepuka kuingiliwa na serikali au mamlaka nyingine yoyote ya nje. FIFA ina haki ya kuchunguza na kuchukua hatua pale ambapo kanuni hizi hazizingatiwi,” inaeleza sehemu ya Katiba ya FIFA.

Maafisa wa FIFA pia watafuatilia kwa karibu mchakato ujao wa uchaguzi, kuhakikisha unaendeshwa kwa haki, uwazi, na kukubalika kimataifa. Timu ya FIFA inatarajiwa kuwepo kufanya tathmini rasmi kufuatia ukaguzi huo, kabla ya kutolewa maamuzi kuhusiana na mustakabali wa TFF.

Wataalamu wa masuala ya michezo wanatafsiri uamuzi huu kuwa ni ishara ya FIFA kutokuwa na imani na mwenendo wa sasa wa uongozi wa TFF, jambo ambalo linaweza kuathiri hadhi ya kimataifa ya soka la Tanzania iwapo hatua madhubuti hazitachukuliwa/FIFA Yatuma Maafisa Tanzania Kufuatilia Migogoro ya TFF.

CHECK ALSO:

  1. Tetesi za Usajili Azam, Muhsin Malima Ajiunga na Azam
  2. Usajili Yanga Leo, Wachezaji Wanaotakiwa na Wananchi
  3. Singida Black Stars Wamtaka Amankona, Kuimarisha Safu ya Ushambuliaji
  4. Florent Ibenge Karibu Kujiunga na Azam kama Kocha Mkuu Mpya