CV ya Jonathan Ngwem wa Simba 2025/2026: Beki wa kushoto raia wa Cameroon, Jonathan Ngwem ameanza mazoezi rasmi na klabu ya Simba Sports Club ya Tanzania, iliyopo nchini Misri kwa ajili ya msimu wa 2025/2026.
Akiwa mchezaji huru kufuatia kumalizika kwa mkataba wake na klabu ya Modern Future FC ya Misri, Ngwem kwa sasa anafanya mazoezi na Wekundu hao wa Msimbazi kwa ajili ya majaribio ya kutathmini ujuzi wake kabla ya kufanya uamuzi wa mwisho kuhusu uhamisho wake.
Kwa mujibu wa habari za ndani ya klabu hiyo, kocha wa Simba SC, Fadlu Davids ndiye anayesimamia majaribio ya Jonathan Ngwem. Iwapo itaridhika na utendaji wake, Simba SC itamsainisha mkataba wa mwaka mmoja/CV ya Jonathan Ngwem wa Simba 2025/2026.

Ngwem mwenye uzoefu wa soka la kimataifa ana uwezo wa kucheza nafasi ya beki wa kushoto na amecheza kwa misimu kadhaa na timu ya taifa ya Cameroon (The Indomitable Lions).
CV ya Jonathan Ngwem wa Simba 2025/2026
Personal information | |||
---|---|---|---|
Full name | Jonathan Joseph Ngwem | ||
Date of birth | 20 July 1991 | ||
Place of birth | Douala, Cameroon | ||
Height | 1.78Â m (5Â ft 10Â in) | ||
Position(s) | Left back | ||
Team information | |||
Current team
|
Simba SC | ||
Number | 13 | ||
Senior career* | |||
Years | Team | Apps | (Gls) |
2011–2012 | Pouma | ||
2013–2014 | Jeunesse Bonamoussadi | ||
2015–2016 | Unisport | ||
2016–2017 | Progresso do Sambizanga | 6 | (1) |
2018 | Unisport | ||
2018–2021 | El Gouna | 82 | (1) |
2021– | Future FC | 11 | (0) |
International career‡ | |||
2015– | Cameroon | 10 | (0) |
Endapo Ngwem atasajiliwa ataongeza ushindani kwenye nafasi ya beki wa kushoto ambayo tayari imeimarishwa na ujio wa Anthony Mligo kutoka Namungo FC. Simba SC inaendelea kuonyesha dhamira ya dhati ya kufikia msimu bora zaidi ndani na nje ya Tanzania.
CHECK ALSO:
Weka maoni yako