Aishi Manula Atua Azam Rasmi Baada ya Miaka 8 Simba

Usajili wa Dirisha Kubwa 2025, Aishi Manula Atua Azam Rasmi Baada ya Miaka 8 Simba | Klabu ya Azam FC imethibitisha kumsajili rasmi golikipa mahiri Aishi Manula ambaye amejiunga na timu hiyo baada ya kuondoka Simba SC aliyoichezea kwa misimu minane mfululizo.

Aishi Manula Atua Azam Rasmi Baada ya Miaka 8 Simba

Kwa mujibu wa taarifa zilizotolewa na klabu hiyo, mkataba huo umesainiwa, picha rasmi za utambulisho zimepigwa, na maandalizi yote ya msimu mpya wa Ligi Kuu Tanzania Bara yamekamilika.

Aishi Manula anatarajiwa kuwa golikipa chaguo la kwanza wa Azam FC kwa msimu wa 2025/2026. Ujio wake ni sehemu ya mikakati ya klabu hiyo kuimarisha kikosi chake kwa nia ya kutwaa mataji ya ligi na mashindano ya kimataifa.

Aishi Manula Atua Azam Rasmi Baada ya Miaka 8 Simba
Aishi Manula Atua Azam Rasmi Baada ya Miaka 8 Simba

Manula ameichezea Simba SC kwa mafanikio makubwa na kutwaa mataji ya ligi, Kombe la FA na kuiwakilisha klabu hiyo katika michuano mbalimbali ya kimataifa ikiwemo Ligi ya Mabingwa Afrika. Kuwepo kwake golini kwa miaka minane kumezua imani kwa mashabiki wengi wa soka nchini.

Ujio wa Aishi Manula unatuma ujumbe wa wazi kuwa Azam FC haijaridhika na nafasi ya pili au ya tatu. Lengo ni moja tu: ubingwa. Manula atakuwa sehemu muhimu ya mafanikio ya timu hiyo msimu ujao.

CHECK ALSO:

  1. Borussia Dortmund Yamsajili Jobe Bellingham Kutoka Sunderland kwa Euro Milioni 33
  2. Kikosi cha Taifa Stars Leo vs Eswatini 11/06/2025
  3. MATOKEO ya Taifa Stars Leo vs Eswatini 11/06/2025 COSAFA Cup
  4. TFF Yakanusha Kudaiwa na Yanga Tsh 200 Milioni