Attohoula Yao Arejea Mazoezini Baada ya Kupona Majeraha | Beki wa kulia wa Yanga SC, Attohoula Yao amerejea mazoezini baada ya kupona majeraha ya goti yaliyomuweka nje kwa muda.
Yao ambaye ni raia wa Ivory Coast 🇨🇮 amerejea kwenye kikosi cha Wananchi lakini ataendelea na mazoezi chini ya uangalizi wa madaktari kabla ya kurejea rasmi uwanjani kwa mechi za kimashindano.

Kurejea kwake ni habari njema kwa Yanga SC kwani ataongeza benchi la ufundi katika safu ya ulinzi kabla ya mechi zijazo za Ligi Kuu Tanzania Bara na mashindano ya kimataifa. Mashabiki wa wananchi wanatarajia kumuona Yao akirejea kwenye kikosi cha kwanza hivi karibuni.
ANGALIA PIA:
Weka maoni yako