Bei Mpya za Mafuta Tanzania Juni 2025, Dar es Salaam Yapunguwa | EWURA Yatangaza Bei Mpya za Mafuta kwa Juni 2025: Dar es Salaam Falls, Mtwara Yaongoza kwa Bei za Juu
Mamlaka ya Udhibiti wa Huduma za Nishati na Maji (EWURA) imetangaza rasmi bei mpya za mafuta zitakazoanza kutumika leo Juni 4, 2025 huku kukiwa na mabadiliko makubwa katika baadhi ya mikoa ambayo ni Dar es Salaam na Mtwara.
Kwa mujibu wa EWURA, bei ya mafuta ya petroli jijini Dar es Salaam imeshuka kutoka shilingi 2,912 hadi shilingi 2,885 kwa lita, dizeli kutoka shilingi 2,859 hadi shilingi 2,826, huku bei ya mafuta ya taa ikibaki shilingi 2,877.
Bei Mpya za Mafuta Tanzania Juni 2025, Dar es Salaam Yapunguwa
Kwa Bandari ya Tanga, bei mpya ni:
- Petroli: Sh2,946
- Dizeli: Sh2,887
- Mafuta ya taa: Sh2,938
Mtwara, ambayo sasa inaongoza kwa kuwa na bei ya juu zaidi nchini, itauza kwa bei zifuatazo:

- Petroli: Sh2,978
- Dizeli: Sh2,918
- Mafuta ya taa: Sh2,969
EWURA imeeleza kuwa kupungua kwa bei katika soko la dunia kumechangia mabadiliko hayo, ambapo kwa mwezi Juni 2025:
- Petroli imeshuka kwa asilimia 0.9
- Dizeli kwa asilimia 3.4
- Mafuta ya taa kwa asilimia 3.7
Hata hivyo, pamoja na kushuka kwa bei za kimataifa, gharama za uagizaji bidhaa zimeongezeka katika baadhi ya bandari, ikiwa ni pamoja na ongezeko la hadi asilimia 51.55 ya mafuta ya petroli kupitia bandari ya Mtwara, na hivyo kuchochea ongezeko la bei mkoani humo.
ANGALIA PIA:
Weka maoni yako