CAF Yaufungulia Uwanja wa Benjamin Mkapa, Simba Kuutumia dhidi ya Al Masry

CAF Yaufungulia Uwanja wa Benjamin Mkapa, Simba Kuutumia dhidi ya Al Masry | Shirikisho la Soka Afrika (CAF) limeidhinisha Uwanja wa Benjamin Mkapa jijini Dar es Salaam kwa robo fainali na nusu fainali ya Ligi ya Mabingwa Afrika (CAF CL) na Kombe la Shirikisho Afrika (CAF CC) msimu wa 2024/2025.

CAF Yaufungulia Uwanja wa Benjamin Mkapa, Simba Kuutumia dhidi ya Al Masry

Uidhinishaji huu ulitolewa kufuatia ukaguzi wa hivi majuzi wa CAF. Hata hivyo, CAF itaendelea kufuatilia uboreshaji unaoendelea wa uwanja huo ili kuhakikisha unakidhi viwango vya kimataifa.

CAF Yaufungulia Uwanja wa Benjamin Mkapa, Simba Kuutumia dhidi ya Al Masry

Simba SC vs Al Masry – Kombe la Shirikisho la CAF, Aprili 9, 2025 Uamuzi huu wa CAF unakuja wakati Tanzania ikiendelea kujiandaa na mchezo muhimu wa kuwania kufuzu hatua ya nusu fainali ya Kombe la Shirikisho Afrika, ambapo Simba SC itamenyana na Al Masry ya Misri Aprili 9, 2025, kwenye Uwanja wa Benjamin Mkapa.

Mashabiki wa soka wanatarajia mechi yenye ushindani mkali, huku Simba SC wakihitaji ushindi ili kutimiza ndoto zao za kutinga hatua ya nusu fainali ya michuano hiyo.

CHECK ALSO: