Etoo Ashinda Kesi Dhidi ya CAF, Arudishwa Kwenye Orodha ya Wagombea CAF | Rais wa Shirikisho la Soka la Cameroon (FECAFOOT), Samuel Eto’o, ameibuka mshindi katika kesi yake dhidi ya Shirikisho la Soka Afrika (CAF) kwenye Mahakama ya Usuluhishi wa Michezo (CAS).
Etoo Ashinda Kesi Dhidi ya CAF, Arudishwa Kwenye Orodha ya Wagombea CAF
Uamuzi wa CAS, uliotolewa leo Machi 7, 2025, mjini Lausanne, Uswisi, umeamua kumuunga mkono Eto’o, ambaye amerejeshwa rasmi kwenye orodha ya wagombea wa Ujumbe wa Kamati ya Utendaji ya CAF. Hii ina maana kuwa atakuwa mgombea tena katika uchaguzi muhimu unaotarajiwa kufanyika katika muda wa siku tano zijazo.
Katika uamuzi huo, CAF imeagizwa kumlipa Eto’o faranga 8,000 za Uswizi kwa gharama za kisheria na kuhakikisha kuwa jina lake linarejeshwa mara moja kwenye orodha ya wagombea.
Uamuzi huo ni ushindi mkubwa kwa Eto’o na Shirikisho la Soka la Cameroon (FECAFOOT), ambao walipinga uamuzi wa CAF wa kumtenga katika mchakato wa uchaguzi.
Kwa sasa, macho yote yapo kwenye uchaguzi wa CAF, ambapo Eto’o ataendelea na kampeni zake za kuwania nafasi ya Ujumbe wa Kamati ya Utendaji ya CAF.
ANGALIA PIA:
Weka maoni yako