Florent Ibenge Karibu Kujiunga na Azam kama Kocha Mkuu Mpya

Florent Ibenge Karibu Kujiunga na Azam kama Kocha Mkuu Mpya | Azam FC ipo katika hatua za mwisho za kumsajili kocha wa kimataifa, Florent Ibenge raia wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC) kuwa kocha mkuu wa timu hiyo. Habari za uhakika zinaeleza kuwa tayari Ibenge alitembelea makao makuu ya klabu hiyo jijini Dar es Salaam Jumamosi.

Florent Ibenge Karibu Kujiunga na Azam kama Kocha Mkuu Mpya

Katika ziara yake hiyo, Ibenge alikutana na viongozi waandamizi wa Azam FC na kuzunguka maeneo ya klabu hiyo. Inasemekana alifurahishwa na mradi wa maendeleo ya kisasa wa klabu, lakini taarifa za kifedha bado zinajadiliwa kabla ya kusainiwa rasmi kwa makubaliano.

Florent Ibenge Karibu Kujiunga na Azam kama Kocha Mkuu Mpya
Florent Ibenge Karibu Kujiunga na Azam kama Kocha Mkuu Mpya

Azam FC imepania kufanya vyema katika msimu ujao wa Ligi Kuu Tanzania Bara na kupata matokeo mazuri kwenye michuano ya Kombe la Shirikisho Afrika, ambapo inalenga kufuzu kwa hatua ya makundi.

Florent Ibenge ni kocha mwenye uzoefu mkubwa barani Afrika, amewahi kuinoa timu ya taifa ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo na AS Vita Club, ambapo alipata sifa nzuri za kimataifa.

CHECK ALSO:

  1. Hatma ya Maxi Nzengeli Yanga, Mkopo Mpya au Ofa Maniema
  2. Raundi ya 29 NBC Ligi Kuu, Mechi Zote Nane Kupigwa Saa 10:00 Jioni Juni 18
  3. Ratiba ya Ligi Kuu NBC Tanzania Bara 2024/2025
  4. Orodha ya Vilabu Bora Afrika CAF 2025 Club Ranking