Habari za Yanga Leo, Viongozi wa Yanga Waitwa TPLB Kuhusu Dabi ya Kariakoo

Habari za Yanga Leo, Viongozi wa Yanga Waitwa TPLB Kuhusu Dabi ya Kariakoo | Wakati mashabiki wa soka wakiendelea kuishi kwa sintofahamu kuhusu mchezo wa Kariakoo derby, Bodi ya Ligi Kuu Tanzania Bara (TPLB) imewaita viongozi wa Yanga kwenye kikao maalum kujiandaa na mechi hiyo.

Habari za Yanga Leo, Viongozi wa Yanga Waitwa TPLB Kuhusu Dabi ya Kariakoo

Kwa mujibu wa taarifa ya Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF), TPLB imeamua kukutana na viongozi wa Yanga, kwa kuwa wao ndio wenyeji wa mechi hiyo iliyopangwa kufanyika Jumamosi Juni 15, 2025.

Mkutano huo umepangwa kufanyika Jumatatu, Juni 9, 2025, Makao Makuu ya TPLB, Ilala, Dar es Salaam. Lengo kuu la mkutano huo ni kupata taarifa rasmi kuhusu maandalizi ya mechi hiyo muhimu, siku saba tu kabla ya tarehe iliyopangwa.

Habari za Yanga Leo, Viongozi wa Yanga Waitwa TPLB Kuhusu Dabi ya Kariakoo
Habari za Yanga Leo, Viongozi wa Yanga Waitwa TPLB Kuhusu Dabi ya Kariakoo

Afisa mmoja wa juu ndani ya TFF amesema:

“Kutakuwa na kikao cha bodi na timu mwenyeji kitakachofanyika Jumatatu Juni 9, 2025, na kuanzia hapo tutajua nini kitaendelea. Hiki ni kikao cha kawaida tu cha maandalizi ya mchezo.”

Katika kikao hicho Yanga imetakiwa kuwasilisha kamati nzima ya utendaji ya klabu hiyo. Miongoni mwa wageni hao ni Rais wa klabu, Mhandisi Hersi Said, makamu wa rais Arafat Haji, na wajumbe wote wa kamati ya utendaji.

CHECK ALSO:

  1. Kikosi cha Taifa Stars vs Madagascar Leo COSAFA 07/06/2025
  2. Matokeo ya Taifa Stars vs Madagascar Leo COSAFA 07/06/2025
  3. Usajili Simba Yamuwinda Kiungo Chipukizi wa Mali Lassine Kouma
  4. Al Ahly Yamtambulisha Zizo, Yajipanga na Kombe la Dunia la Vilabu 2025