Hatma ya Dabi Iliyoahirishwa Yajulikana Leo, Majibu Kamili ya Kamati

Hatma ya Dabi Iliyoahirishwa Yajulikana Leo, Majibu Kamili ya Kamati | Serikali, TFF, Bodi ya Ligi, Simba SC, na Yanga SC wakutana kujadili mustakabali wa mchezo wa derby ulioahirishwa.

Hatma ya Dabi Iliyoahirishwa Yajulikana Leo, Majibu Kamili ya Kamati

Leo saa nne asubuhi, Serikali kupitia Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo kwa kushirikiana na Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF), Bodi ya Ligi na viongozi wa klabu za Simba SC na Yanga SC watakutana kujadili mustakabali wa mchezo wa derby ulioahirishwa Machi 8.

Kikao cha majadiliano kinatarajiwa kufanyika katika ofisi za Wizara ya Michezo na Baraza la Michezo la Taifa (BMT) ndani ya Uwanja wa Benjamin Mkapa. Lengo kuu la mkutano huu ni kupata mwafaka kuhusu lini na jinsi mchezo utakavyopangwa upya, na wadau wote wanatarajiwa kutoa maoni yao kuhusu mazingira ya mechi hii muhimu.

Hatma ya Dabi Iliyoahirishwa Yajulikana Leo, Majibu Kamili ya Kamati

Mechi kati ya Simba SC na Yanga SC ni moja ya mechi zinazosisimua nchini, hivyo uamuzi utakaotolewa kwenye kikao hiki utakuwa muhimu kwa mustakabali wa Ligi Kuu Tanzania Bara (NBC Premier League).

Endelea kuwa nasi kwa taarifa zaidi kuhusu maamuzi yatakayotolewa katika kikao hiki.

CHECK ALSO: