Kagera Sugar Yasonga Robo Fainali ya CRDB Federation Cup Baada ya Kuiondoa Tabora United: Timu ya Kagera Sugar imefanikiwa kutinga hatua ya robo fainali ya michuano ya CRDB Federation Cup baada ya kuifunga Tabora United kwa mikwaju ya penati 5-3.
Kagera Sugar Yasonga Robo Fainali ya CRDB Federation Cup
Mchezo huo uliopigwa kwenye Uwanja wa Ali Hassan Mwinyi mjini Tabora, ulimalizika kwa sare ya bao 1-1 baada ya muda wa kawaida.
Katika mchezo huo, timu zote zilionyesha ushindani mkubwa, huku Tabora United ikitumia vyema faida ya nyumbani. Hata hivyo, Kagera Sugar walifanikiwa kufunga mchezo huo kwa mafanikio baada ya kushinda kwa mikwaju ya penalti na kutinga hatua inayofuata ya michuano hiyo.
Kwa matokeo hayo Kagera Sugar inaungana na timu nyingine zilizofuzu hatua ya robo fainali ya michuano hiyo inayoendelea kuwavutia mashabiki wengi wa soka nchini Tanzania.

CHECK ALSO:
Weka maoni yako